Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameanza kuchora ramani yake kuelekea hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA kutoka Ethiopia.
Yanga wataanzania ugenini dhidi ya Wenyeji wao hao CBE SA, Septemba 13 na 20 kurudiana Tanzania na mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa visiwani Zanzibar kwa mujibu wa Rais ya Yanga, Hersi Said.
Hatua hiyo ni baada ya Jumamosi Agosti 24, kufanikiwa kuvuka hatua ya mkondo wa kwanza jumla ya ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Vital’o katika michezo miwili waliocheza ya Afrika.
Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kutumia nafasi na bado wana kazi ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo kwa mchezo unaofuata.
Amesema mchezo unaofuata watacheza dhidi ya CBE FC, kabla ya kucheza mchezo huo watakuwa na kibarua katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo wanahitaji kushinda.
“Nimeridhishwa na kiwango cha leo (Jumamosi Agosti 24) hivi ndio tunavyotakiwa kuwatendea haki mashabiki. Bado tunaendelea na kazi hatua inayofuata tutacheza na CBE,” amesema Kocha huyo wa Yanga.
Amesema wanahitaji ushindi katika michezo hiyo wa kujipanga kuelekea hatua inayofuata kwa kumfatilia ubora wa mpinzani wake anapokuwa nyumbani na ugenini.
Gamondi amesema wanatumia michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kujiimarisha zaidi na kutafuta matokeo chanya kwa kufikia malengo yao ya kutetea mataji hayo.
Katika hatua nyingine Hersi amesema wako kwenye mipango ya mechi yao ya marudiano dhidi ya CBE SA kwenda kucheza katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
"Kulingana na vigezo vya Shirikisho la mpira wa miguu Ulimwenguni (FIFA), tunatarajia kwenda kucheza visiwani Zanzibar mechi zetu zijazo," amesema Hersi.
Yanga inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Agosti 29 uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.