BAADA YA KUFUZU NUSU KIBINGWA ....ZIMBWE Jr 'ATEMA BUNGO' SIMBA....ATAJA WALICHOFANYA


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


BEKI tegemeo wa klabu ya Simba, Mohammed Hussein maarufu kama Zimbwe JR, ametamka kwa kujiamini kuwa kikosi cha msimu huu ni bora zaidi kuwahi kuchezewa tangu ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi.
 
Akizungumza kwa msisitizo, Zimbwe JR amesema kuwa takwimu hazidanganyi licha ya kucheza kwenye vikosi vingi vya Simba, timu ya sasa imefanya makubwa kwa kufuzu hadi hatua ya nusu fainali ya mashindano ya kimataifa, jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi.
 
“Kuna Simba bora niliyowahi kuchezea, lakini hii ya sasa ni ya kipekee.
Tumefuzu nusu fainali baada ya miaka mingi ya kujaribu kuandika historia. Mwaka 1993 ilikuwa ni historia inayozungumzwa sana lakini sasa nasi tumeandika yetu,” amesema kwa furaha.
 
Zimbwe JR amefichua kuwa mafanikio hayo hayakutokea kwa bahati nasibu.
Anaeleza kuwa kila kitu kilianza tangu mechi ya kwanza walipowasili nchini Misri, ambapo walifanya kikao kizito na kocha wao Fadlu Davids.
 
“Mazungumzo kati yetu na kocha yalikuwa na uzito. Kocha alieleza malengo kutoka robo fainali hadi nusu fainali. Sote tulijitolea kupigania hilo, na leo hii tumefanikisha,” alisema beki huyo.
 
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 04/11/2025