MAXI NZENGELI ALIVYOIPELEKA YANGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


KIUNGO wa Yanga, Maxi Nzengeli ameweka wazi kulingana na program wanayopewa na Kocha Miguel Angel Gamondi ni suala la muda kukata kiu ya mashabiki wao kuona timu yao ikicheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
 
Yanga ili wafanikiwe kutinga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo wanatakiwa kuhakikisha wanaiondoa Al Merrikh, mchezo unaofuata wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Septemba 16, mwaka huu.
 
 
Max alisema malengo yao ni kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kufikia malengo yao ya kufika hatua ya makundi.
 
 
Alisema  malengo yake  anaisaidia Yanga kufika kwenye malengo kwenye michuano hiyo kwa kufika katika hatua ya makundi huku akiamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwaondoa Al Merrikh.
 
 
“Malengo ya timu ndio ya wachezaji wote, kwetu tunatamani kuona tunafika makundi na kupita zaidi ya hapo,  kikubwa tunachokifanya kwa sasa ni kuona tunapambana zaidi kwenye michezo yetu.
 
 
“Kocha anaendelea kufanya majukumu yake ya kuendelea kufanyia kazi makosa aliyoyaona kwenye mechi zilizopita, tunashinda michezo yetu miwili iliyo mbele yetu dhidi ya Al Merrikh,” alisema Nzengeli.
 
 
 
Alisema muhimu zaidi kwa upande wetu kuona wanafanya vizuri na kupata matokeo, kuna uwezo huo na tutapambana zaidi kufikia malengo yao .
 
 
Nzengeli alisema anaimani ya timu yake kufanya vizuri katika mashindano ya ligi ya Mabingwa Afrika na kuona Yanga ikitinga makundi kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 09/13/2023