BEKI wa Simba, Hennock Inonga hatokuwa sehemu ya mechi ya marudiano ya
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia ya kufuatia kushonwa nyuzi 13 katika katika jeraha alilopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union.
Inonga alishindwa kuendelea na mchezo huo juzi baada ya kuumizwa na winga wa Coastal Union, Hija Ugando dakika 20 kulisababisha kuchanika juu kidogo ya kifundo cha mguu.
Kwa mujibu wa Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alisema baada ya tukio hilo alikimbizwa hospital ya Rufaa ya Temeke kwa ajili ya matibabu kwa kupelekea kushonwa nyuzi 13 katika jeraha hilo na tayari ameruhusiwa kurudi nyumbani.
“Inonga ameruhusiwa kutoka Hospital amepata jeraha pale pale alipoumia katika mechi iliyopita na Tanzania Prisons, jambo zuri ni kwamba hajavunjika mfupa ni kidonda tu.
"Suala atakaa nje kwa muda gani inategemea na jinsi atakavyopona lakinj haikuwa sehemu mbaya sana aliyoumia,” alisema Daktari huyo wa Simba.
Naye Mwanachama wa Chama cha Madaktari wa michezo Tanzania (TASMA) Cosmas Kapiga alieleza kuwa beki huyo hatakaa nje kwa muda mrefu kulingana na jeraha alilopata.
Alisema kitaalamu kuwa mtu yeyote ambaye ameshona anatakiwa kukaa siku saba anatolia nyuzi, baada ya hapo kidonda kupona inachukuwa siku 7 hadi
14 ndani ya siku hizo kudonda kitaanza kupona.
“Lakini kwa jeraha la Inonga kwa kuwa amepata shida kwenye mguu mmoja
basi baada ya kuondolewa nyuzi anaweza kufanya mazoezi ya kujiweka
sawa bila mguu uliopata shinda kuusumbua
"Baada ya siku 14 hizo ndio atatakiwa kufanya mazoezi ya kusukumana na wenzake kwa kuwa tayari kidonda kimepona,” alisema Kapinga aliyewahi kuwa Daktari wa Simba na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya tiba ya Shirikisho la Riadhaa Tanzania.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.