EPL - Wolverhampton Wanderers v Liverpool FC 


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 Premier League
Matchday 5

Wolverhampton Wanderers v Liverpool FC 

Molineux Stadium 
Wolverhampton, West Midlands, England
Saturday, 16 September 2023 
Kick-off is at 13h30 
 
Wolverhampton Wanderers na Liverpool watakabiliana kwenye mechi ya ligi ugani Molineux mnamo Septemba 16.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
Wolves walipoteza mechi yao ya mwisho ya ligi 3-2 dhidi ya Crystal Palace ugenini Septemba 3 ambao ulikuwa ni mchezo wao wa pili kupoteza katika michezo mitatu ya ligi iliyopita.  
 
Vile vile, Wolves hawajashinda mchezo wowote katika mechi mbili zilizopita za ligi wakiwa nyumbani huku wakipoteza mechi moja na kupata sare moja ugani Molineux.
 
Kwingineko Liverpool waliishinda Aston Villa 3-0 wakiwa nyumbani Septemba 3 na kufikisha idadi ya mechi 15 za ligi bila kushindwa.
 
The Reds vile vile hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi saba zilizopita ugenini huku wakiandikisha sare tatu na kushinda mechi nne.
 
Vikosi
 
Joseph Hodge ni mchezaji wa pekee anayeuguza jeraha kwa upande wa Wolves na hawana mchezaji anayetumikia marufuku au adhabu.
 
Liverpool watakosa huduma za mlinzi Virgil van Dijk anayetumikia marufuku, Trent Alexander-Arnold, Thiago Alcantara na Ibrahim Konate wanaouguza majeraha.
 
Nukuu
 
"Wachezaji wengi watakuwa wakitumikia timu za taifa na kisha watarudi kuendeleza juhudi,” alisema mlinzi wa Liverpool Joe Gomez baada ya ushindi dhidi ya Villa.
 
"Tutazidi kujituma. Kumekuwa na mabadiliko mengi mwaka huu. Wachezaji wapya wameonyesha uwezo mkubwa na juhudi si haba.
 
"Umekuwa ni mwanzo mpya na inafurahisha kuona wachezaji wapya wakijumuika vizuri na kikosi kipya na kuonyesha uwezo wao. Huu ni mwanzo tu ila tutazidi kujituma.”
 
Takwimu baina ya timu hizi
 
Liverpool waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Wolves walipokutana mara ya mwisho katika mechi ya ligi Machi 1 2023 ugani Anfield.
 
Wolves walikuwa wamevunja msururu wa mechi 11 bila kushinda dhidi ya Liverpool katika mechi ya mkondo wa kwanza wa msimu 2022/23 kabla ya mechi hiyo.
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 4.


Septemba 16 Jumamosi

2:30pm - Wolverhampton Wanderers v Liverpool FC
5:00pm - Aston Villa v Crystal Palace
5:00pm - Fulham FC v Luton Town
5:00pm - Manchester United v Brighton & Hove Albion
5:00pm - Tottenham Hotspur v Sheffield United
5:00pm - West Ham United v Manchester City
7:30pm - Newcastle United v Brentford FC

Septemba 17 Jumapili

4:00pm - AFC Bournemouth v Chelsea FC
6:30pm - Everton FC v Arsenal FC

Septemba 18 Jumatatu

9:45pm - Nottingham Forest v Burnley FC

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 09/13/2023