Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 6
Manchester City v Nottingham Forest
Etihad Stadium
Manchester, England
Saturday, 23 September 2023
Kick-off is at 17h00
Manchester City wanatarajia kushinda
mchezo wao wa sita wa ligi mfululizo tangu kuanza kwa msimu huu mpya watakapoialika Nottingham Forest ugani Etihad Jumamosi Septemba 23.
City ambao ni mabingwa watetezi wameshinda mechi zote tano msimu huu huku mchezo wao wa mwisho ukiwa ni ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham London Stadium Septemba 16.
Vijana wa Pep Guardiola wanazidi kuongoza ligi alama mbili mbele ya Tottenham, Liverpool na Arsenal mtawalia huku timu hizo zikipishana kwa ubora wa mabao tu baada ya kushinda mechi zao wikendi iliyopita.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Forest walitoka nyuma na kuzawazisha katika mechi iliyoishia sare ya 1-1 dhidi ya Burnley mnamo Septemba 18 na sasa wanashikilia nafasi nane kwenye msimamo wa ligi.
Forest wameanza msimu huu vizuri ukilinganisha na msimu uliopita ambapo walijizolea alama tatu tu katika michezo mitano ya kwanza ya msimu baada ya kupoteza 6-0 mikononi kwa City.
Forest chini ya Steve Cooper wapo alama sita juu ya nafasi za kushushwa daraja, huku Sheffield United, Burnley na Luton wakishikilia nafasi ya 18, 19 na 20 mtawalia.
Erling Haaland alifunga magoli matatu maarufu kama hat-trick dhidi ya Forest msimu uliopita na anatarajia kupata idadi zaidi ya magoli baada ya kuanza msimu huu kwa kishindo. Raia huyo wa Norway tayari amefunga magoli saba katika mechi tano msimu huu ikiwa ni pamoja na magoli matatu dhidi Fulham Septemba 2.
Taiwo Awoniyi amefanikiwa kufunga magoli matatu na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili katika michezo mitano. Mshambuliaji huyo raia wa Nigeria amefunga katika mechi saba za ligi mfululizo na kumuweka miongoni mwa wachezaji wachache kutoka Afrika kufanya hivyo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Guardiola alizungumzia umuhimu wa wachezaji Kyle Walker na Bernardo Silva walio ongeza mkataba na kikosi hicho.
Ilkay Gundogan na Riyad Mahrez waliondoka City na kujiunga na timu zingine baada ya kukamilika kwa msimu jana. Pep alikiri kuwa kuondoka kwa Walker na Silva kungeathiri kikosi chake vibaya.
"Kumpteza Kyle na Bernardo kungetuathiri vibaya mno,” alisema Guardiola. "Sio tu kwa sababu ya ubora uwanjani, bali pia wana sifa za kipekee na mchango mkubwa kwa njia tofauti.
"Inahitaji mwaka mmoja, miwili, mitatu au zaidi kuwa na sifa kama hizo na kuchukua nafasi ya wachezaji watakao ondoka. Wana uwezo huo.
"Sio rahisi kupata sifa kama za Bernardo na Walker. Inahitaji muda kuzipata. Lilikuwa jambo la busara kusalia hasa baada ya Gundo na Riyad kuondoka.
"Tumeshawapoteza wachezaji watatu. Kuwapoteza wengine wawili ingekuwa hasara kubwa. Tuna furaha sana kuwa klabu imeamua kuwaongezea mkataba na wanataka kuwa nasi.”
Cooper alisifia wachezaji wake kwa kuonyesha ushujaa wao dhidi ya Burnely ambapo Callum Hudson-Odoi alifunga goli la kusawazisha baada ya Zeki Amdouni kufunga goli la dakika ya 41.
"Tuliruhusu goli kutokana na uzembe. Tulifanya mabadiliko machache na kujituma baada ya kosa hilo na kuonyesha uwezo wetu,” alisema.
"Goli la Callum linaashiria uwezo wake. Nahisi tulicheza vizuri na nia ya kushinda mechi hiyo. Tulipata goli na mchezo ukafunguka.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi – 5
Man City - 1
Forest - 2
Sare - 1
Ratiba ya ligi ya Premier League mchezo wa 6:
Jumamosi, Septemba 23
5:00pm: Crystal Palace v Fulham
5:00pm: Luton Town v Wolverhampton Wanderers
5:00pm: Manchester City v Nottingham Forest
7:30pm: Brentford v Everton
10:00pm: Burnley v Manchester United
Jumapili, Septemba 24
4:00pm: Arsenal v Tottenham Hotspur
4:00pm: Brighton & Hove Albion v Bournemouth
4:00pm: Chelsea v Aston Villa
4:00pm: Liverpool v West Ham United
6:30pm: Sheffield United v Newcastle United
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.