EPL - Bournemouth v Arsenal


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 English Premier League
Matchday 7

Bournemouth v Arsenal

Vitality Stadium
Bournemouth, England
Saturday, 30 September 2023
Saa 4:00pm jioni, Majira ya Afrika ya Kati
 
Arsenal wanatarija kupata ushindi watakapokutana na Bournemouth katika mechi ya ligi ugani Vitality Jumamosi Septemba 30.
 
The Gunners walitoka sare ya 2-2 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Tottenham katika mechi ya ligi ya 194 baina ya timu hizo iliyochezwa Septemba 24.
 
Hata hivyo, sare hiyo ilifikisha kikomo msururu wa ushindi wa mechi mbili mfululizo kwa Arsenal, ikiwa ni baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United na 1-0 dhidi ya Everton na sasa wapo katika nafasi ya tano, alama nne nyuma ya viongozi Manchester City.
 
Brighton wanashikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la ligi baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya the Cherries Septemba 24 huku Liverpool wakiwa wa pili baada ya ushindi wa 3-1 dhidi  ya West Ham saa 24 baadaye.
 
Dominic Solanke of BournemouthHakimiliki ya picha: Getty Images

 
Baada ya kupoteza dhidi ya Brighton, Bournemouth wanashikilia nafasi ya 17, alama 2 juu ya nafasi za kushushwa daraja.
 
Kabla ya mechi dhidi Brighton, Bournemouth chini ya Andoni Iraola walikuwa wametoa sare mbili; dhidi ya Brentford (2-2) na Chelsea (0-0) lakini nafasi ya kupata ushindi dhidi ya Arsenal ni finyu mno baada ya kupoteza mechi zote mbili dhidi ya wapinzani hao msimu uliopita, na jumla ya mechi sita zilizopita za ligi baina yao pasi na ushindi.  
 
Hata hivyo, the Cherries wamefanikiwa kufunga goli katika mechi nne kati ya sita zilizopita huku Dominic Solanke akipata goli dhidi ya West Ham, the Bees na Albion. 
 
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alihusika na magoli 13 kati ya magoli 37 ya ligi ya klabu hiyo msimu 2022-23 na anaonekana kuwa katika hali nzuri msimu huu ikiwa amefunga magoli 3 na kusaidia lingine moja tayari.

Bukayo Saka
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Bukayo Saka amekuwa na mchango mkubwa kwa timu ya Arsenal msimu huu huku aakiwa na magoli matatu baada ya mechi sita. Msimu uliopita, mchezaji huyo mwenye miaka 22 alikuwa na msimu wa kufana; akifanikiwa kufunga magoli 14 na kusaidia mengine 11.
 
Iraola alishuhudia timu yake ikicheza na ujasiri mkubwa katika kipindi cha kwanza dhidi ya Brighton na kukiri kuwa tofauti baina ya timu hizo ni kuwa Brighton walitumia nafasi zao na kufunga magoli.
 
"Nahisi tulicheza mchezo mzuri kipindi cha kwanza. Sio rahisi kuwadhibiti Brighton hasa wakiwa nyumbani kama tulivyofanya sisi. Tuliwalazimisha kucheza katika nusu yao ya uwanja katika kipindi cha kwanza,” Raia huyo wa Uhispania aliambia AFCB TV.
 
"Walikuwa na mchezo mzuri katika kipindi cha pili na kutumia nafasi walizozipata. Licha ya kupata nafasi, hatukuweza kufunga na kusawazisha mchezo.”
 
Arteta alionyesha kutoridhishwa kwake na matokeo dhidi ya Tottenham huku akisema timu yake ingeibuka na ushindi iwapo wangekuwa watulivu na kutumia nafasi zao vilivyo.
 
"Hatujafurahi kutokupata alama zote tatu hasa baada ya kutangulia kufunga mara mbili na njia ya uzembe tuliyo ruhusu magoli,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Tulikuwa tumeudhibiti mchezo na tungeongeza magoli zaidi. Tulifunga goli na kuruhusu goli katika kipindi cha dakika moja.
 
"Tukio hili liliathiri sana timu kimawazo. Tulikosa utulivu wa kutoa pasi muhimu kuelekeza eneo la wapinzani.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Bournemouth - 0
Arsenal – 4
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 7:

 
Septemba 30 Jumamosi
2:30pm: Aston Villa v Brighton & Hove Albion
5:00pm: Bournemouth v Arsenal
5:00pm: Everton v Luton Town
5:00pm: Manchester United v Crystal Palace
5:00pm: Newcastle United v Burnley
5:00pm: West Ham United v Sheffield United
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Manchester City
7:30pm: Tottenham Hotspur v Liverpool
 
Oktoba 1 Jumapili
4:00pm: Nottingham Forest v Brentford
 
Oktoba 2 Jumatatu
10:00pm: Fulham v Chelsea

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 09/29/2023