AFCON - Algeria v Tanzania 


Alamy Hisa Picha


2023 Africa Cup of Nations Qualifiers

Algeria v Tanzania 

Group F
19 May 1956 Stadium
Annaba, Algeria
Referee: Djindo Louis Houngnandande (Benin)
Thursday, 7 September 2023
Kick-off is at 21h00  
 
Algeria itakuwa mwenyeji wa Tanzania katika mechi ya kufuzu shindano la mataifa bingwa barani Afrika (AFCON) 2023, mnamo Septemba 7 ugani 19 May 1956.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
Algeria, maarufu kama the Desert Foxes, tayari wamefuzu kushiriki shindano hilo baada ya kuishinda Uganda 2-1 ugenini Juni 18 katika mechi ya mwisho ya kundi F.  
 
Algeria hawajapoteza mechi hata moja katika mechi 13 za kufuzu AFCON zilizopita na vile vile kucheza mechi 19 za kufuzu bila kupoteza yoyote wakiwa nyumbani.
 
Tanzania watafuzu kushiriki fainali hizo za 2023 iwapo wataibuka na ushindi dhidi ya Algeria. Hii ni baada ya kuwashinda 1-0 Niger katika mechi ya mwisho ya kundi F mnamo Juni 18.
 
Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars hawajapoteza mchezo wowote katika michezo miwili ya kufuzu iliyopita.
 
Wachezaji wa kutegemea.
 
Riyad Mahrez ambaye ni nahodha wa Algeria amefungia timu ya taifa magoli 30 katika michezo 83, anatarajiwa kuwa na mchango mkubwa iwapo Algeria itahitaji kushinda mechi hii.
 
Tanzania wataweka matumaini yao kwa nahodha na mshambuliaji Ally Samatta ambaye amefanikiwa kufunga magoli 22 katika mechi 63.
 
Nukuu
 
"Nitafanya mabadiliko kwenye kikosi kabla ya mechi yetu na Algeria,” alisema kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Adel Amrouche.
 
"Kuna wachezaji ambao hawajafika ila nimefurahishwa na juhudi za tulionao.
 
"Tunahitaji wachezaji wanaojituma. Kuzingatia hilo, kuna wachezaji katika kikosi hiki ambao hawatoshiriki mechi dhidi ya Algeria.”
 

Takwimu baina ya timu hizi

 
Timu hizi mbili zimekutana mara 12 katika mashindano yote tangu Januari 1973.
 
Algeria wameshinda mechi saba dhidi ya moja kwa faida ya Tanzania huku mechi nne zikiishia sare.
 
The Desert Foxes waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Taifa Stars walipokutana mara ya mwisho, ambayo ilikuwa ni mechi ya kufuzu AFCON 2023 Juni 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 09/06/2023