Verstappen apania ushindi wa Dutch GP kwa mara nyingine


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship

2022 Dutch Grand Prix

Circuit Zandvoort
North Holland, Netherlands
Sunday, 4 September 2022
 
Dereva wa Red Bull Racing Max Verstappen anatarajia kuendeleza ubabe wake kwenye mashindano ya mbio za magari za dunia za Formula One msimu katika mbio za Dutch Grand Prix Jumapili Septemba 4.
 
Verstappen ambaye ni bingwa wa sasa wa dunia wa mashindano hayo amefanikiwa kupata ushindi katika mbio tisa kati ya mbio 14 za msimu huu. Amekosa nafasi za jukwaani mara tatu tu msimu huu na mara kati ya hizo ilitokana na matatizo za kiufundi ya gari lake.

Sergio Perez
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Ushindi wa mbio za Belgian Grand Prix wikendi iliyopita ulikuwa wa nne mfululizo kwa Verstappen ambaye aliweka nafasi ya alama 91 kati yake na dereva mwenza ambaye alimaliza katika nafasi ya pili kwenye mkondo Circuit de Spa-Francorchamps.
 
Raia huyo wa Uholanzi vile vile aliibuka na ushindi kwenye mkondo wa Circuit Zandvoort mwaka uliopita baada ya mbio hizo kurejea nchini Uholanzi kwa mara ya kwanza tangu 1985.

Carlo Sainz Jr
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Verstappen alionyesha uwezo wake wa kucheza na magurudumu kwa uzuri kwenye mbio za Spa na anahisi kuwa hiyo ni sifa ambayo ni silaha kubwa katika uendeshaji wake.
 
"Sio leo tu. Nimeonyesha uwezo wangu wa kuendesha bila kujali mazingira na hali ya magurudumu. Nafikiri watu hawatilii maanani hilo,” alisema dereva huyo mwenye umri wa miaka 24 baada ya mbio hizo.
 
"Muhimu zaidi ni uzoefu na kuhakikisha unaweka gari lako kwenye hali nzuri. Wakati mwingine unafanikiwa na wakati mwingine utafeli kufanya hivyo.
 
"Ukiangalia kwa mfano, hatukuwa na mbio nzuri Austria lakini tulijifunza mengi na ambayo yalitusaidia kwenye mbio zilizofuata.”
 

Matokeo ya mbio za Belgian Grand Prix 2022.

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Sergio Perez - Red Bull Racing
Nafasi ya tatu: Carlos Sainz - Ferrari
 

Aposta na MotoGP com a Betway

 

Apostar no automobilismo com a Betway é rápido e emocionante. Com acesso a uma grande variedade de mercados e odds, não vai demorar muito para apostar a 100 km/h. Clica AQUI para registar uma nova conta e aproveita a nossa oferta de boas-vindas de até 5,000 MT em apostas grátis. A oferta de boas-vindas pode ser usada para apostar na Fórmula 1, MotoGP, NASCAR ou qualquer desporto da tua escolha.


 
Para as mais recentes notícias sobre desporto, dicas de aposta e promoções, siga a Betway no FacebookTwitter, e Instagram. Baixa o aplicativo da Betway.

Published: 09/01/2022