Dortmund wahaha jinsi ya kumdhibiti Haaland


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022/23 UEFA Champions League

Group stage
Matchday 2

Manchester City v Borussia Dortmund

Etihad Stadium
Manchester, England
Wednesday, 14 September 2022
 
Erling Haaland anatarajia kuendeleza ubabe wake dhidi ya waajiri wake wa zamani Dortmund, watakapokutana kwenye mechi ya UEFA Champions League siku ya Jumatano Septemba 14.
 
Hii ni miezi miwili tangu Halaand kuighura Dortimund kwa kima cha paini milioni sitini kwenda ligi ya premier na kujiunga na mabingwa City baada ya miaka miwili Signal Iduna Park.
 
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanikiwa kufunga magoli 86 katika mechi 89 kwenye mashindano yote akiwa na Dortimund na anaonekana kuendeleza makali hayo Uingereza kwani tayari ameshafunga magoli 12 katika mechi nane kwa faida ya City.
 
Kevin de Bruyne of Manchester City
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

Alifunga magoli mawili kwenye mechi ya kwanza ya UEFA msimu huu City ilipoishinda Sevilla 4-0 nchini Uhispania na kumiminiwa sifa nyingi na kiungo Kevin de Bruyne aliyepata tuzo ya mchezaji wa bora wa mechi.
 
"Najitahidi sana kufanya kazi yang una kujiweka kwenye maeneo mazuri na kutengeneza nafasi nzuri,” alisema De Bruyne. "Kwa namna moja ama nyingine Erling atakutana nazo. Kwa sasa anafunga magoli na ameanza ligi hii kwa kishindo.
 
"Ameingiana na ligi hii vizuri kwa maoni yangu lakini pia nje ya uwanja kuna mambo zaidi ambayo ni changamoto.
 
'Akiendelea na hali hiyo na kufunga mabao itakuwa ni faida kwetu.”
 
Vile vile, BVB walianza vizuri katika mechi zao za Ulaya baada ya kupata ushindi wa 3-0 nyumbani dhidi FC Copenhagen ugani Signal Iduna Park wiki iliyopita.
 
Hata hivyo, wamekuwa na matokeo mseto kwenye mechi za ligi na wanakutana na City baada ya kupoteza 3-0 dhidi ya RB Leipzig Jumamosi iliyopita, ambayo ilikuwa mechi ya pili kupoteza katika mechi sita.
 
Borussia Dortmund head coach Edin Terzic
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

Kocha mkuu wa Dortmund Edin Terzic alikiri kuwa vijana wake walikuwa na wakati mgumu kudhibiti mbinu za timu hiyo ya Red Bulls na wanafaa kujiandaa zaidi kwa mbinu kama hizo dhidi ya the Citizens ambao huo ndio mtindo wao wa kucheza.
 
"Tulikuwa na wakati mgumu dhidi ya mtindo wao wa kucheza. Hatukuweza kushambulia vyema. Tuliacha kujiamini na kuruhusu magoli kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika." Terzic said.
 
"Hatukucheza vizuri dhidi ya mpinzani mzuri. Hatukustahimili shinikizo lao na kudhibiti mtindo huo mara kwa mara."
 

Takwimu baina ya timu hizi:

Mechi - 4
Man City - 2
Dortmund - 1
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 09/14/2022