Quartararo atazamia ushindi wa kwanza wa mbio za Aragon MotoGP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

2022 Aragon Grand Prix

Round 15
MotorLand Aragón
Alcañiz, Spain 
Sunday, 18 September 2022
 
Fabio Quartararo anatazamia kushinda mbio za Aragon Grand Prix kwa mara ya kwanza na kuvunja msururu wa mbio nne bila ushindi.
 
Mwendeshaji huyo wa Yamaha alikuwa na mbio za zisizo za kuridhisha za Aragon Grand Prix mwaka jana alipomaliza kwenye nafasi ya nane.
 
Quartararo hajapata ushindi katika mbio nne zilizopita zikijumuisha mbio za hivi maajuzi za San Marino MotoGP Septemba 4 alipomaliza kwenye nafasi ya tano.

Franco Morbidelli of Yamaha
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa nyuma ya mwendeshaji wa Ducati Luca Marini huku akifukuzia nafasi ya nne lakini alikosa nafasi hiyo kwa muda mchache sana na kumaliza katika nafasi ya tano.
 
Mwendeshaji wa Ducati Francesco Bagnaia aliibuka na ushindi wa mbio za San Marino MotoGP huku Enea Bastianini wa Ducati na Maverick Vinales wa Aprilia wakichukua nafasi ya pili na tatu mtawalia.  
 
Licha ya kuwa na mbio za kutamausha hivi karibuni, Quartararo anaongoza kwenye jedwali la 2022 la waendeshaji huku akitarajia kutetea taji lake la dunia.
 
Iwapo atashinda mbio za Aragon MotoGP, Quartararo atapanua uongozi wake kwenye jedwali huku zikisalia mbio sita msimu huu kukamilika.
 
"Mbio hizi hazikuwa rahisi,” alisema Quartararo ambaye ni raia wa kwanza kutoka Ufaransa kuwa bingwa wa mashindano haya katika historia baada ya mbio za San Marino MotoGP. 
 
"Zilikuwa ni mbio za kwanza nilizokuwa nyuma ya pikipiki nyingine bila kuwa na tatizo la gurudumu la mbele.
 
"Nilikuwa na kasi sawia na niliyokuwa nayo kwenye mbio za mazoezi. Ukiwa nyuma ya mpinzani inakuwa sio hali nzuri kama inavyokuwa ukiendesha peke yako,” aliongezea.
 
"Tulipata nafasi ya tano ambayo tulistahili leo. Nilijaribu kadri ya uwezo wangu.”
 
Ducati wanaongoza kwenye jedwali la kampuni huku wakifuatiwa na Yamaha na kisha Aprilia wanashika nafasi ya tatu..
 

Matokeo ya mbio za Aragon MotoGP 2021

 
Mshindi: Francesco Bagnaia - Ducati 
Nafasi ya pili: Marc Marquez - Honda 
Nafasi ya tatu: Joan Mir - Suzuki 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 09/16/2022