Mbio za Italian Grand Prix 2022 kung’oa nanga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

16 Round

2022 Italian Grand Prix

Monza Circuit
Monza, Italy
Sunday, 11 September 2022
 
Mbio za magari za Italian Grand Prix 2022 zinatarajiwa kung’oa nanga Monza ambao ni mji uliopo eneo la Lombardy Italia Septemba 11. 
 
Hizi zitakuwa mbio za 16 za msimu wa 2022 FIA za dunia na zitaandaliwa kwenye mkondo wa Monza Circuit. 
 
Pamoja na British Grand Prix, Monza ni mkondo ambao umekuwa ukiandaa mbio za dunia za Formula one kila msimu tangu mashindano haya yalipobuniwa mwaka 1950. 
 
Mbio za hivi karibuni za msimu 2022 FIA Formula One zilikuwa Dutch Grand Prix mnamo Septemba 4 ambapo Max Verstappen aliibuka na ushindi.

George Russell
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Dereva wa Mercede George Russell na Charles Leclerc wa Ferrari walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye mkondo Circuit Zandvoort.
 
Verstappen anaendelea kuonyesha ubabe wake na bado yupo kileleni mwa jedwali 2022 la madereva baada ya kujizolea alama 310. 
 
Charles Leclerc wa Ferrari na alama 201, na Sergio Perez wa Red Bull Racing-RBPT Perez na alama 201 wanashikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye jedwali.
 
Russell 188, Carlos Sainz Jr wa Ferrari 175 na Hamilton 158 wanashikilia nafasi ya nne, tano na sita mtawalia. 

Carlo Sainz Jr
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Mapokezi yamekuwa mazuri hapa. Madereva wote tunajihisi vizuri kushiriki mbio za mkondo Zandvoort hapa Uholanzi," Russell alisema baada ya mbio za Dutch Grand Prix.
 
"Kwa pamoja kama timu tulikuwa na kasi nzuri japokuwa matokeo siyo tuliyotarajia. Matokeo hayo yatatusaidia kuimarika katika mbio zijazo. 
 
"Inafurahisha kuwa na wawakilishi watatu tofauti katika jukwaa. Timu yetu ya Mercedes, hatua kwa hatua tunakaribia kileleni. Tuzidi kupambana.” 
 
Red Bull Racing-RBPT wanaongoza kwenye jedwali la waundaji huku wakifuatiwa na Ferrari kisha Mercedes wanachukua nafasi ya tatu. 
 

Matokeo ya mbio za Italian Grand Prix 2021

 
Mshindi: Daniel Ricciardo - McLaren-Mercedes 
Nafasi ya pili: Lando Norris - McLaren-Mercedes 
Nafasi ya tatu: Valtteri Bottas - Mercedes 
 

Aposta na MotoGP com a Betway

 

Apostar no automobilismo com a Betway é rápido e emocionante. Com acesso a uma grande variedade de mercados e odds, não vai demorar muito para apostar a 100 km/h. Clica AQUI para registar uma nova conta e aproveita a nossa oferta de boas-vindas de até 5,000 MT em apostas grátis. A oferta de boas-vindas pode ser usada para apostar na Fórmula 1, MotoGP, NASCAR ou qualquer desporto da tua escolha.


 
Para as mais recentes notícias sobre desporto, dicas de aposta e promoções, siga a Betway no FacebookTwitter, e Instagram. Baixa o aplicativo da Betway.


 
 

Published: 09/09/2022