Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 4
Real Madrid v Real Betis
Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain
Saturday, 3 September 2022
Kick-off is at 17h15
Real Madrid na Real Betis watamenyana ugani Estadio Santiago Bernabéu katika
mechi ya ligi kuu Uhispania mnamo Septemba 3.
Madrid walipata ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya RCD Espanyol kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Agosti 28.
Madrid hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi sita za mwisho walizocheza baada ya kuandikisha ushindi kwenye mechi tano na sare moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Madrid hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi nne walizocheza nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara tatu mfululizo na sare moja ugani Estadio Santiago Bernabeu.
"Kwa kawaida, wengi wanategemea tutakuwa na ugumu kwenye mechi za ugenini. Tulidhibiti mechi hadi walipofunga goli. Dakika za mwisho thelathini tulianza tena kudhibiti mechi,” alisema kiungo wa Madrid Toni Kroos baada ya ushindi dhidi ya Espanyol.
"Walianza kuonyesha uchovu na tukatumia nafasi hiyo kuwadhibiti. Kupata ushindi wa ugenini sio rahisi na tumefanikiwa kufanya hivyo kwenye mechi tatu mfululizo. Tunajivunia hilo. Ni muhimu kujituma zaidi hata pale unapoishiwa nguvu.
"Wapinzani wetu wana wachezaji wazuri wenye vipaji. Tutakumbana na hali hii kila baada ya siku nne kutoka leo na kwenda mbele. Tutalazimika kuzama zaidi na juhudi za ziada nyakati nyingine na tuna uzoefu huo.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwengineko, Betis walipata ushindi wa 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya CA Osasuna kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi Agosti 16.
The Green and Whites hawajashindwa katika mechi yoyote ya ligi kati ya mechi tano za mwisho walizocheza huku wakiandikisha ushindi mara tano na sare moja.
Vile vile, Betis hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi saba za mwisho wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare nne na kushinda mechi tatu kama wageni.
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya timu hizi ilikuwa mwezi Mei 20 2022.
Mchezo huo uliishia sare ya 0-0 na ulichezewa ugani Estadio Santiago Bernabeu.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Madrid - 2
Betis - 2
Sare - 1
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wanne.
Septemba 2 Ijumaa
10:00pm - Celta Vigo v Cadiz CF
Septemba 3 Jumamosi
3:00pm - Real Mallorca v Girona FC
5:15pm - Real Madrid v Real Betis
7:30pm - Real Sociedad v Atletico Madrid
10:00pm - Sevilla FC v FC Barcelona
Septemba 4 Jumapili
3:00pm - CA Osasuna v Rayo Vallecano
5:15pm - Athletic Bilbao v RCD Espanyol
7:30pm - Villarreal CF v Elche CF
10:00pm- Valencia CF v Getafe CF
Septemba 5 Jumatatu
10:00pm - Real Valladolid v UD Almeria
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.