Inter wapania ushindi dhidi ya Torino


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 6

Inter Milan v Torino FC

Stadio Giuseppe Meazza 
Milano, Italy 
Saturday, 10 September 2022
Kick-off is at 18h00 CAT 
 
Inter Milan watakuwa mwenyeji wa Torino FC kwenye mechi ya ligi ugani Stadio Giuseppe Meazza mnamo Septemba 10.
 
The Big Grass Snake walipoteza 3-2 ugenini dhidi ya AC Milan kwenye mechi iliyopita ya ligi ya Septemba 3.
 
Hii ilikuwa mechi ya pili ya ligi ya Inter Milan kupoteza huku wakipata ushindi dhidi ya US Cremonese kabla ya kukabiliana na Milan.

Simone Inzaghi - Inter manager
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Inter Milan hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi nane zilizopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara saba na kupata sare moja ugani Stadio Giuseppe Meazza.
 
“Sioni ulinganisho wowote na mechi tuliyopoteza Stadio Olimpico lakini kuna kipindi tulipunguza kasi yetu na tukaadhibiwa magoli matatu,” meneja wa Inter Simone Inzaghi baada ya mechi dhidi ya Milan. 
 
"Ni muhimu sana kudhibiti mchezo nyakati tofauti. Hatuwezi kupotea kwenye mechi kama tulivyotokea dhidi ya Milan na Lazio. Mambo madogo kwenye baadhi ya mechi yana maana kubwa. 
 
“Inaumiza kupoteza mchezo huu wa dabi. Una maana kubwa kwetu. Tulikuwa na nafasi ya kujituma zaidi. Inauma sana. Tumewaangusha mashabiki na klabu yetu.” 

Sasa LukicHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko Torino walichapwa 3-1 ugenini dhidi ya Atalanta BC kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi mnamo Septemba 1 na wataalika US Lecce on Septemba 5.
 
Matokeo hayo yalifikisha kikomo msururu wa mechi tatu bila kushindwa kwa Torino huku wakiandikisha sare moja na kushinda mechi mbili. 
 
Vile vile, kupoteza dhidi ya Atalanta kulifikisha kikomo msururu wa mechi saba za ligi bila kushindwa wakiwa ugenini baada ya kuandikisha ushindi mara tano na kupata sare mbili. 
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Inter na Torino ilikuwa Machi 13 2022.
 
Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 na ilichezewa ugani Stadio Olimpico Grande Torino ulio na uwezo wa mashabiki 27,958.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Inter - 4
Torino - 0
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi ya Serie A mchezo wa sita

  
Septemba 10 Jumamosi
 
4:00pm - SSC Napoli v Specia Calcio 
 
7:00pm - Inter Milan v Torino FC 
 
9:45pm - AC Milan v UC Sampdoria 
 
Septemba 11 Jumapili
 
13:30pm - Atalanta BC v US Cremonese 
 
6:00pm - Bologna FC v ACF Fiorentina 
 
6:00pm - US Lecce v AC Monza 
 
6:00pm - US Sassuolo v Udinese Calcio 
 
7:00pm - SS Lazio v Hellans Verona
 
9:45pm - Juventus FC vs Salermnitana 
 
Septemba 12 Jumatatu
 
9:45pm - Empoli FC v AS Roma 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 09/08/2022