England watamani ushindi wa kwanza dhidi ya Italia tangu 2012


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Nations League

League A - Group 3
Matchday 5

Italy v England

Stadio Giuseppe Meazza
Milan, Italy
Friday, 23 September 2022
Kick-off is at 21h45  
 
England wanatamani kupata ushindi wao wa kwanza kwenye ligi ya UEFA Nations League watakapomenyana na Italia ugani San Siro Ijumaa Septemba 23.
 
The Three Lions wamekuwa na mwanzo mbaya kwenye mashindano haya huku wakifanikiwa kupata alama mbili katika mechi nne za kwanza za kundi la 3.
 
Katika hali ya kushangaza, vijana wa Gareth Southgate walipata kichapo mara mbili mikononi mwa Hungary huku mechi ya mwisho dhidi ya taifa hilo ikiishia 4-0 Wolverhampton kwenye mchezo wa nne.
 
England ambao walifika fainali ya mashindano ya mataifa bingwa Ulaya 2020 wamefanikiwa kufunga goli moja kwenye mechi za kundi lao, ambapo ilikuwa mechi dhidi ya Ujerumani (1-1) mnamo Juni 7.

Roberto Mancini
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Southgate ana uchu wa kuongoza kikosi chake kupata matokeo mazuri na kusahau matokeo mabaya ya miezi mitatu iliyopita huku wakijeweka tayari kwa ajili ya kombe la dunia 2022 kwa kupambana dhidi ya mabingwa wa Ulaya.
 
"Ukiwa kocha wa timu ya taifa hakuna mechi zinazokuja kwa haraka kusaidia kurekebisha makosa ya mechi zilizopita,” alisema.
 
"Tumekuwa na muda mrefu wa kujitathmini lakini sasa tuna mechi mbili kubwa zitakazo tuwezesha kupima uwezo wetu na kutusaidia kujiandaa kwa ajili ya kombe la dunia. Tuna wiki nane tu kutaja kikosi cha kombe la dunia Qatar kwa hivyo tunafaa kutumia kila sekunde vilivyo.”
 
The Azzurri walishuhudia msururu wao bila kupoteza mechi yoyote ukifika kikomo baada ya kushindwa 5-2 na Ujerumani kule Monchengladback kwenye mechi ya mwisho ya shindano hili.

Hata hivyo, timu ya Roberto Mancini ina uwezo wa kuibuka na ushindi wa kundi hilo kwani wapo nyuma ya Hungary kwa alama mbili huku zikisalia mechi mbili tu.  
 
"Matokeo mazuri ni muhimu. Chochote chaweza kutokea katika soka. Sharti tujitume kushinda mechi zote mbili. Nina wachezaj wachanga na walio na uzoefu,” alisema Mancini kwenye kikao na waandishi wa habari.
 
"Hakuna raha kupoteza mechi 5-2 lakini pia niliona mambo mazuri kwenye mechi hiyo. Mechi kama hii wakati mwingine zinakusaidia kujiimarisha. Ilikuwa ni mechi ya tano mfululizo iliyokuja mwishoni mwa msimu. Wachezaji wachanga wamepata uzoefu na tumefanikiwa alama tano.”
 

Takwimu baina ya timu hizi

Mechi - 29
Italia - 12
England - 8
Sare - 9

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 09/22/2022