Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 9
Manchester City v Manchester United
Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 2 October 2022
Kick-off is at 16h00
Manchester City wanatarajia kupata ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya United watakapokutana kwenye
mechi ya 188 baina yao Jumapili Oktoba 2.
City walipata ushindi kwenye mechi mbili za ligi dhidi ya United msimu uliopita; 2-0 ugani Old Trafford na 4-1 katika uwanja wa Etihad miezi minne baadaye.
Vijana wa Pep Guardiola hawajapoteza mechi yoyote msimu huu japokuwa walipoteza alama nne baada ya kutoka sare ya 3-3 na 1-1 dhidi ya Newcastle na Aston Villa mtawalia.
The Citizens walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Wolves ugani Molineux kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi na wapo katika nafasi ya pili, alama moja nyuma ya viongozi Arsenal baada ya mechi saba.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Pep Guardiola alionekana kufurahishwa na uchezaji wa sajili mpya Manuel Akanji baada ya kucheza dakika tisini za kwanza na klabu hiyo.
"Ni mchezo mzuri sana anayetumia maarifa; kwenye pasi fupi au ndefu. Sio mwepesi wa kusababisha mipira ya adhabu au penalti,” alisema raia huyo wa Uhispania akimzungumzia Akanji.
"Anajituma sana anapokabiliana na mpinzani na anafanya hivyo kwa utulivu. Ni mchezaji mzuri zaidi.”
Mambo yanaonekana kuwaendea vizuri The Red Devils chini ya ukufunzi wa Ten Hag baada ya kuwa na mwanzo mbaya wa msimu walipopoteza mechi mbili za kwanza mfululizo dhidi ya Brighton na Brentford.
Hata hivyo, Ten Hag amewezesha timu hiyo kuimarisha matokeo yao kwa kushinda mechi nne zilizofuata ikiwemo ushindi wa 3-1 dhidi ya viongozi wa ligi, Arsenal.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa sasa, United wapo alama tano nyuma ya majirani wao City huku wakiwa na mechi moja mkononi. Ten Hag ana imani hakuna mchezaji wa kikosi chake atakayepata jeraha kipindi cha mapumziko.
"Mapumziko hay ani muhimu sana. Tunapata muda wa kuwa na mikutano ya jinsi ya kuimarisha utendakazi wa klabu,” alisema raia huyo wa Uholanzi.
"Nafasi kama hizi zinakuwepo baada ya mechi. Sharti tuwe tayari lakini asilimia tisini ya wachezaji wameitwa kwenye vikosi vya taifa. Tutafanya mazoezi na wachezaji waliosalia.
"Ni matumaini yangu kila mchezaji atarudi mzima wa afya bila jeraha lolote.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Man City - 2
Man United - 2
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.