Verstappen atazamia kuushangaza ulimwengu Urusi


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021 Formula 1 Ubingwa wa Dunia

Mkondo wa 15

Russian Grand Prix

Sochi Autodrom
Jumapili, 26 Septemba 2021
15:00 
 
Max Verstappen anatazamia kupata matokeo yasiyotarajiwa na atakaposhiriki mkondo wa 15 wa mashindano ya mbio za magari ya Formula 1 Ubingwa wa Dunia 2021, the Russian Grand Prix, katika mzunguko wa Sochi Autodrom Jumapili 26 Septemba.
 
Dereva huyo wa Red Bull Racing-Honda danaongoza msimamo wa madereva akiwa na lama 226.5, huku dereva wa Mercedes Lewis Hamilton akimfuata kwa karibu sana alama 221.5. Madereva hao wawili walipambana vikali katika mashindano ya Italia Grand Prix mapema mwezi huu, wakagongana kwenye kona ya pili ya shindano, gari la Verstappen likapanda juu ya lile la Hamilton wote wakalazimika kuyaacha mashindano.

Lewis Hamilton
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Verstappen alipewa adhabu ya kufungiwa nafasi tatu za kwanza katika kuanza mashindano kutokana na mchango wake katika ajali hiyo, hii ikimaanisha ataweza tu kuanzia kwenye nafasi ya nne au nje zaidi kwenye mashindano ya Russian GP. 
 
Bingwa wa zamani wa F1 Jacques Villeneuve amewashtumu wasimamizi mjini Monza kwa adhabu aliyopewa dereva huyo Mholanzi, akitoa tetesi kuwa adhabu kama hiyo hiyo itawatia hofu madereva wasikaribiane sana wakati wa mashindano.
 
“Walimuadhibu Verstapen kwa sababu gari la Red Bull lilipanda juu ya kichwa cha Hamilton. Unapata adhabu kwa ajili ya matokeo, na sio kwa ajili ya kitendo chenyewe, ilhali siku zote wanasema athari haina umuhimu,” alisema Mkanada huyo.  

Sergio Perez
Hakimiliki ya picha: Getty Images 


“Verstappen siku zote anatumia nguvu, lakini Hamilton naye hutumia nguvu zaidi. Halafu ukiwakutanisha wote wawili kwenye kona, wanazidisha. Lakini matukio kama hayo ni sehemu ya Formula 1. Mkianza kutoa adhabu za aina hii kila wakati, madereva hawatakimbia tena kwa sababu wataogopa kupita wenzao.”
 
Mkuu wa timu ya Red Bull Racing-Honda Christian Horner aliongeza, “Tumekasirishwa na adhabu ya kufungiwa nafasi tatu za kwanza katika kuanza, lakini tumekubali uamuzi wa wasimamizi. Kilichotokea kati ya Max na Lewis, kwa maoni yetu, ni ajali ya kawaida kwenye mashindano.
 
“Unaweza kuwatetea wote wawili, lakini inavunja moyo kuona magari yote mawili yakiondoka kwenye mashindano yanayosisimua."
 

Msimamo wa Madereva

1 – Max Verstappen, Red Bull Racing-Honda, alama 226.5 
2 – Lewis Hamilton, Mercedes, alama 221.5
3 – Valtteri Bottas, Mercedes, alama 141
4 – Lando Norris, McLaren-Mercedes, 132
5 – Sergio Perez, Red Bull Racing-Honda, 118
 

Msimamo wa Timu

1 – Mercedes, alama 362.5 
2 – Red Bull Racing-Honda, 344.5
3 – McLaren-Mercedes, 215
4 – Ferrari, 201.5
5 – Alpine-Renault, 95

 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/24/2021