Verstappen apania ushindi anaporejea Dutch GP


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Ubingwa wa FIA Formula One 2021 

2021 Dutch Grand Prix

Circuit Zandvoort
Zandvoort, Uholanzi 
Jumapili, 5 Septemba 2021
 
Dereva wa Red Bull Racing-Honda Max Verstappen atakuwa anapania ushindi atakaposhiriki kwenye mashindano ya Dutch Grand Prix.
 
Dereva huyo mwenye umri wa miaka 23 ni mwanawe Jos Verstappen, dereva wa zamani wa Formula One nchini Uholanzi, na anadhamiria kutwaa ushindi kwa heshima ya baba yake.
 
Verstappen alianza kupata ushindi tena kwenye mashindano ya hivi karibuni ya Belgian Grand Prix mnamo tarehe 29 Agosti, akatwaa ushindi katika nchi alikozaliwa mama yake.
 
Lando Norris of McLaren (Lando Norris wa McLaren)
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

George Russell wa timu ya Williams alipanda jukwaani la washindi kwa mara ya kwanza alipomaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya Verstappen. 
 
Naye bingwa wa dunia wa Formula One Lewis Hamilton alimaliza katika nafasi ya tatu, huku akionekana kuelekea kufanikiwa kutetea taji hilo.
 
Kwenye msimamo wa madereva mwaka huu, Hamilton yuko kileleni akifuatwa na  Verstappen, na nafasi ya tatu inashikiliwa na Lando Norris wa timu ya McLaren-Mercedes.
 
Verstappen yuko nyuma ya Hamilton kwa alama tatu tu, na huenda akaongoza msimamo ikiwa atashinda mashidano ya mwishoni mwa wiki ya Dutch Grand Prix.
 
Lewis Hamilton of Mercedes (Lewis Hamilton wa Mercedes )
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

"Ilikuwa vigumu kudhibiti gari na kwa sababu mvua ilinyesha alasiri yote hali haikuimarika," Verstappen alisema baada ya kushinda Belgian Grand Prix
 
"Nadhani leo hongera kubwa ni kwa mashabiki waliokaa kando ya mzunguko mchana kutwa kwenye mvua, upepo, na baridi. Lazima ilikuwa mateso kukaa katika hali hiyo.
 
"Kwa hivyo nawashukuru wote na wao kwa hakika ndio washindi leo. Sasa lazima tuendelee kujituma na kujaribu kurejea katika uongozi," aliendelea. 
 
"Nina uhakika tuna gari nzuri na bado safari ni ndefu kwa hivyo tunahitaji tu kuhakikisha tunapata matokeo bora kabisa sehemu ya msimu iliyobakia."
 
Mercedes wanaongoza upande wa timu wakifuatiwa na Red Bull Racing-Honda katika nafasi ya pili, huku McLaren-Mercedes wakiwa katika nafasi ya tatu.
 

Matokeo ya Dutch Grand Prix 1985

 
Mshindi: Niki Lauda - McLaren-TAG
Nafasi ya pili: Alain Prost - McLaren-TAG  
Nafasi ya tatu: Ayrton Senna - Lotus-Renault
 

Bashiri Formula 1 na Betway

Bashiri mbio za langa langa na Betway. Ujionee machaguo mengi na odds nono, haitochukua muda mrefu kabla ya kubashiri 100km/h. Bonyeza HAPA kujisajili na akaunti mpya na daka Free Bet TSh 3,000 ambayo unaweza kutumia kubashiri kwenye Formula 1, Moto GP, NASCAR au mchezo wowote wa chaguo lako.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

 

Published: 09/02/2021