Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 Formula 1 Ubingwa wa Dunia
Mkondo wa 14
Italian Grand Prix
Autodromo Nazionale di Monza
Jumapili, 12 Septemba 2021
14:00
Max Verstappen anatazamia kuendelea kukaa kileleni katika mashindano ya mbio za magari ya Formula 1 Ubingwa wa Dunia, kwenye mkondo wa 14 wa mashindano hayo yatakayofanyika katika mzunguko wa the Autodromo Nazionale di Monza jumapili tarehe 12 Septemba alasiri.
Verstappen alichukua nafasi ya juu katika msimamo wa madereva alipoibuka mshindi kiulaini kwenye mashindano ya Dutch Grand Prix mjini Zandvoort mwishoni mwa wiki iliyopita, akafikisha alama 224.5- akimzidi Lewis Hamilton wa Mercedes (221.5) kwa alama tatu pekee.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Nashindwa kuelezea kwa maneno," alisema dereva huyo mwenye umri wa miaka 23 baada ya ushindi mbele ya mashabiki wa nyumbani. “Walikuwa na matarajio makubwa kutoka kwangu wikendi hii, lakini tulifaulu.
Imekuwa wiki nzuri sana. Unahitaji gari ili kuibuka mshindi, na tulifanikiwa- tulikuwa na gari nzuri. Tulifaulu, na zilikuwa juhudi za pamoja.”
Hata hivyo, mjini Monza itakuwa changamoto ngumu zaidi, kwa sababu mzunguko huo maarufu, siku za nyuma umewafaa zaidi madereva wa Mercedes ambao wanakuwa na kasi kubwa kwenye sehemu zilizonyooka; ingawa Verstappen anaamini timu yao ya Red Bulls itafanya bidii kupambana na Mercedes, wanaojulikana kwa jina la utani ‘Silver Arrows’.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Ni wepesi sana kwenye sehemu zilizonyooka. Na mimi pia nina kasi, lakini sio kama wao. Lakini tutaweka bidii za ziada kukomboa muda wanaotuzidi nao kwa kasi yao, na tutajaribu kujituma kwa dhati,” alisema Mholanzi huyo.
Verstappen atakuwa anatafuta ushindi wa tatu ndani ya wikendi tatu, baada ya kutwaa ushindi kwa nusu alama kwenye mashindano ya Belgian Grand Prix ambayo yalivurugwa na mvua mwishoni mwa mwezi Agosti.
Akifanikiwa kufanya hivyo, itakuwa ni mara ya pili kutwaa ushindi mara tatu mtawalia msimu huu, kwa sababu alikuwa tayari ameshinda mara tatu mfululizo mashindano ya French Grand Prix, Styrian Grand Prix na Austrian Grands Prix mwezi Juni na Julai.
Msimamo wa Madereva katika Mashindano
1 – Max Verstappen, Red Bull Racing-Honda, alama 224.5
2 – Lewis Hamilton, Mercedes, alama 221.5
3 – Valtteri Bottas, Mercedes, 123
4 – Lando Norris, McLaren-Mercedes, 114
5 – Sergio Perez, Red Bull Racing-Honda, 108
Msimamo wa Timu
1 – Mercedes, alama 344.5
2 – Red Bull Racing-Honda, 332.5
3 – Ferrari, 181.5
4 – McLaren-Mercedes, 170
5 – Alpine-Renault, 90
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway