Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya Italia- Serie A
Wiki ya 7
Torino FC v Juventus FC
Stadio Olimpico Grande Torino
Torino, Italia
Jumamosi, 02 Octoba 2021
Kuanzia 19h00
Torino FC itapimana nguvu na mahasimu wao wa mjini, Juventus FC katika ligi kuu ya Italia -
Serie A kwenye uwanja wa Stadio Olimpico Grande Torino Octoba 02.
The Maroons waliweza kuwabana Venezia sare ya 1-1 ugenini mchezo wa karibuni katika ligi hiyo mnamo Septemba 27.
Sare hiyo iliendeleza msururu wa matokeo ya kutoshindwa kwa Torino kufikia mechi nne wakiwa wameandikisha ushindi mara mbili mtawalia na sare mbili.
Torino hawajapoteza katika mechi mbili walizocheza nyumbani karibuni kwenye Serie A, wakiwa wameandikisha sare moja na kupata ushindi mara moja katika Stadio Olimpico Grande Torino.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
.
Wakati huo huo, Juventus walipata ushindi wa 3-2 baada ya pambano kali dhidi ya Sampdoria mechi yay a karibuni katika Serie A, mnamo Septemba 26.
Kwa matokeo hayo yana maana Yuve hawajapoteza katika mechi tatu za karibuni kwenye ligi hiyo wakiwa wameandikisha sare moja na ushindi mara mbili mfululizo.
Juventus iliwafunga Spezia mechi ya mwisho ugenini katika Serie A, ushindi uliomaliza ukame wa mechi mbili bila ushindi ugenini.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Tulicheza vizuri nusu ya kwanza, inasikitisha kuhusu goli hilo tulilofungwa, na tunaomba msamaha. Hata hivyo, tulirejea uwanjani tukiwa na Imani kubwa," nyota wa Juventus Federico Bernardeschi alisema baada ya mchezo huo dhidi ya Sampdoria.
"Tunahitaji kujituma zaidi ili kuhakikisha ushindi mapema, na kukataa kuwaruhusu wapinzani wetu kubadili mambo. Ninapocheza kushoto inabidi nifanye kazi tofauti na ile ninayofanya upande ule mwingine wa uwanja, kutoa usaidizi zaidi na pia kulinda.
"Kushangiliwa na mashabiki nilipokuwa napimzishwa ilinipa raha sana. Ikiwezekan, niko tayari pia kucheza mbele, tunaona uamuzi kocha [Massimiliano Allegri] atakaotoa."
Mchezo wa mara ya mwisho kati ya Torino na Juventus ulikuwa Aprili 3, 2021.
Timu hizo zilitoka sare 2-2 mechi iliyofanyika katyika uwanja wa Stadio Olimpico Grande Torino.
Takwimu (Mechi tatu za karibuni Serie A)
Mechi - 3
Torino - 0
Juventus - 3
Sare- 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway