Spurs na Chelsea kuwasha Derby ya London


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Ligi Kuu ya England

Siku ya 5 kati ya 38

Tottenham Hotspur vs Chelsea 

Tottenham Hotspur Stadium 
London, England
Jumapili, 19 Septemba 2021
Inaanza 18:30
 
Tottenham Hotspur watawakaribisha Chelsea Jumapili hii katika mechi ya ligi kuu ya England 2021/22 inayotarajiwa kuwa derby ya London ya kusisimua sana.

Harry Kane
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Spurs waliandikisha ushindi wa 1-0 dhidi ya Watford mechi yao ya kufungua msimu kabla ya kufungwa 3-0 na Crystal Palace mwishoni mwa wiki iliyopita. Kadi nyekundu aliyoonyeshwa Japhet Tanganga iliacha pengo la kufungwa magoli katika uwanja wa Selhurst Park huku meneja mpya Nuno Espirito Santo akipoteza mechi ya kwanza ya ligi tangu alipochukua mikoba.
 
Huku kukiwa bado kuna maswali mengi kuhusu uwezo wa Tottenham msimu huu, Chelsea wanaonekana ni miongoni mwa washindani wa taji.
 
The Blues walishinda michezo mitatu ya kwanza ya msimu huu na kuwabana Liverpool sare ya 1-1 uwanjani Anfield licha ya kucheza sehemu kubwa ya mtanange huo wakiwa na wachezaji 10. Pamoja na ngome imara ya ulinzi, wana safu ya ushambuliaji inayozidi kuimarika ikiongozwa na Romelu Lukaku.
 
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji amerejea Chelsea tena, na alifunga magoli mawili katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Aston Villa mechi yao ya mwisho.
 
"Yeye [Lukaku] ni nyongeza ya thamani, mwenye haiba ya kufana, na sihitaji kuzungumzia zaidi kuhusu yeye ni mchezaji wa aina gani. Alidhihirisha hilo katika timu zote alizochezea. Ni mchezaji muhimu sana kwetu na tunatumai ataendelea hivyo," alisema kiungo wa Chelsea Mateo Kovacic alipoulizwa kuhusu mwenzake.  

"Ilikuwa mechi ngumu dhidi ya Aston Villa lakini mwishowe tulifanikiwa kushinda 3-0 na kudhihirisha umahiri wa kikosi chetu” aliongeza

Mateo Kovacic
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Chelsea walizoa alama nne kutoka kwa Spurs msimu uliopita. Sare ya 0-0 katika Stamford Bridge ilifuatiwa na ushindi wa 1-0 kaskazini mwa London ambapo Jorginho alifunga goli hilo la ushindi kupitia mkwaju wa penalti.
 

Takwimu za Tottenham Hotspur vs Chelsea

 
Mechi zilizochezwa: 152
Tottenham Hotspur wakashinda: 49
Chelsea wakashinda : 66
Sare : 37
 

Ratiba ya Mechi za Ligi kuu ya England, wiki ya 5,

 
Ijumaa, 17 Septemba 
 
22:00 - Newcastle United vs Leeds United 
 
Jumamosi, 18 Septemba 
 
14:30 - Wolverhampton Wanderers vs Brentford 
17:00 - Norwich City vs Watford 
17:00 - Burnley vs Arsenal 
17:00 - Manchester City vs Southampton 
17:00 - Liverpool vs Crystal Palace 
19:30 - Aston Villa vs Everton 
 
Jumapili, 19 Septemba 
 
16:00 - Brighton & Hove Albion vs Leicester City 
16:00 - West Ham United vs Manchester United 
18:30 - Tottenham Hotspur vs Chelsea 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/15/2021