Sevilla yalenga kuiokomesha Barcelona


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Ligi kuu ya Uhispania

Wiki ya 4

Sevilla FC v FC Barcelona 

Estadio Ramón Sánchez Pizjuán
Sevilla, Uhispania 
Jumamosi, Septemba 11, 2021
  
Sevilla FC itakutana na FC Barcelona kwenye ligi kuu ya Uhispania katika uwanja wa Estadio Ramón Sánchez Pizjuán jumamosi Septemba 11. 
  
Sevilla, kwa jina la utani Los Palanganas walibanwa sare ya 1-1 na Elche ugenini mechi ya ligi ya karibuni mnamo Agosti 28.
  
Sare hiyo iliwawezesha Sevilla kufikisha idadi ya mechi nne bila kupoteza katika ligi, wakiwa wameshinda tatu mtawalia na kutoka sare mara moja.
  
Lucas Ocampos
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
Los Palangana pia hawajapoteza nyumbani katika mechi tatu za La Liga walizocheza, wameshinda tatu mtawalia.
  
Wakati huo huo, Barcelona walipata ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya Getafe nyumbani mechi waliocheza mara ya mwisho katika ligi iliyochezwa Agosti 29.
  
Kwa ushindi ushindi huo Barca walifikisha idadi ya mechi nne bila kupoteza katika ligi hii wakiwa wameshinda tatu na kutoka sare moja.
  
Barcelona pia hawajapoteza katika mechi tano za ugenini zilizopita kwenye La Liga wakiwa wameandikisha sare mbili na ushindi mara tatu ugenini.
  
Ronald Koeman – Meneja wa Barcelona
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
"Katika mechi kama ya leo, msimu uliopita tulipoteza alama na leo tumeshinda [dhidi ya Getafe]. Hii ni muhimu sana," Ronald Koeman, meneja wa Barcelona alisema. 
  
"Nimefurahia sana alama tatu. Ulikuwa mchezo mgumu na tunajua jinsi ya kuumia. Hatujawa wazuri kwenye umiliki wa mpira.  
  
"Kisaikolojia imekuwa muhimu kwetu. Tunajua jinsi ya kujituma na kucheza kwa nia ya kushinda."
  
Mara ya mwisho Sevilla na Barcelona kukutana ilikuwa Februarui 27, 2021.
  
Barcelona waliwalemea sana Sevilla wakashinda 2-0 mechi iliyochezewa katika Estadio Ramón Sánchez Pizjuán.
  

Takwimu (Mechi tano zilizopita)


Mechi - 5
Sevilla - 0
Barcelona - 3
Sare - 2
 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 09/08/2021