Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 MotoGP – Msimu wa Ubingwa wa Dunia
Aragon MotoGP
Mkondo wa 13
MotorLand Aragón
Alcañiz, Uhispania
Jumapili, Septemba 12, 2021
Mwendeshaji wa timu ya Yamaha Fabian Quartararo atakuwa anatazamia kushinda kwa mara ya pili mfululizo atakaposhiriki mashindano ya mbio za pikipiki ya Aragon
MotoGP.
Mwendeshaji huyo mahiri kutoka Ufaransa hakupata matokeo mazuri katika mashindano hayo ya Aragon mwaka uliopita kwani alimaliza kwenye nafasi ya 18 na akakosa kuzoa alama hata moja.
Hata hivyo, Quartararo anaonyesha kujiamini sana baada ya kushinda mashindano ya hivi karibuni msimu huu yaliyofanyika katika British MotoGP mnamo Agosti 29.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Alex Rins wa Suzuki alimaliza wa pili nyuma ya Quartararo na ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda kwenye jukwaa la washindi msimu huu.
Naye Mwispania Aleix Espargaro alimaliza katika nafasi ya tatu, akaweka historia ya kuwa mwendeshaji wa kwanza wa timu ya Aprilia kumaliza miongoni mwa watatu wa kwanza wanaopanda jukwaani.
Kwenye msimamo wa waendeshaji, Joan Mir wa Suzuki na Johann Zarco wa timu ya Ducati wako kwenye nafasi ya pili na tatu kwa utaratibu huo, huku wakipambana kumfikia kiongozi Quartararo.
Quartararo kwa sasa anamzidi Mir kwa alama 65 na atakaribia kushinda ubingwa wa dunia wa MotoGP ikiwa atashinda mashindano ya Aragon MotoGP.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Wakati wa mashindano nilijisikia niko vizuri," Quartararo alisema baada ya mashindano ya British Grand Prix na alisisitiza hafikirii kuhusu kushinda taji la dunia la MotoGP.
"Nawapita hatua kwa hatua na ilikuwa vyema.Kisha kasi yangu ilikuwa ya nguvu sana, sikutarajia kuwaacha wapinzani. Nilifurahia mwendo kasi mzuri lakini sikwenda asilimia 100.”
"Ni safari ndefu. Siwazi kuhusu hilo hata kidogo kwa sasa hivi na ndivyo unavyofanikiwa kuongeza alama kuwazidi wapinzani.
"Kwa sasa furaha imenizidi, najisikia vizuri sana ninapopanda pikipiki.”
Yamaha wako kileleni upande wa timu, Ducati kwenye nafasi ya pili na KTM katika nafasi ya tatu.
Matokeo ya Aragon MotoGP 2020
Mshindi: Alex Rins - Suzuki
Nafasi ya pili: Alex Marquez - Honda
Nafasi ya Ttau: Joan Mir - Suzuki
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway