PSG, Man City kukutana Ubingwa wa Ulaya


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Ligi ya Klabu Bingwa

KUNDI A

Paris Saint Germain (PSG) v Manchester City 

Parc des Princes
Paris, Ufaransa
Jumanne, 28 Septemer 2021
Inaanza 22h00 
 
Paris Saint Germain (PSG) itapambana na Manchester City mechi ya kundi A, Ligi ya klabu Bingwa Ulaya mnamo Septemba 28.
 
Wababe hao wa Ufaransa walibanwa sare ya 1-1 na mabingwa wa ubelgiji Club Brugge ugenini mechi yao ya karibuni katika kundi A tarehe 15 Septemba.
 
Sare hiyo iliongeza idadi ya michezo ambayo PSG wamekosa ushindi mfululizo kufikia minne katika Ligi ya Klabu bingwa Ulaya, wakiwa wamepoteza mechi tatu na kutoka sare mara moja.

Neymar
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Wafaransa hao wamekosa ushindi katika mechi tatu za karibuni walizocheza nyumbani kwenye michuano hiyo, wakiwa wameandikisha sare moja na kupoteza mara mbili mtawalia.
 
Wakati huo huo, City walipata ushindi wa 6-3 dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani wakichezea nyumbani mechi ya karibuni kundi A tarehe 15 Septemba.
 
Ushindi huo ulikuwa hatua kubwa ya city kuanza tena kupata matokeo mazuri katika ubingwa wa Ulaya baada ya wapinzani wao Chelsea kupoteza mara ya kwanza ndani ya 1mechi 2 bila kushinda katika ligi hiyo.
 
City pia hawajapoteza katika mechi 10 za ugenini kwenye michuano hiyo wakiwa wameandikisha sare mbili na kupata ushindi mara nane.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
“Ndio maana naridhika kabisa na wachezaji kwa ushindi wao wa kwanza kwenye hatua ya makundi," Meneja wa Man City Pep Guardiola alisema baada ya ushindi wao dhidi ya Leipzig. 
 
“Bila shaka nimefurahi sana, na nawashukuru wachezaji hawa hodari tulio nao. Ilikuwa mechi ngumu. Ilikuwa muhimu sana kupata ushindi mchezo wa kwanza nyumbani na tulifunga mabao sita.
 
“Nadhani mchezo ulikuwa mgumu. Tulibahatika kufunga punde tu baada ya wao kutufunga. Magoli tisa ndani ya mechi moja, ni raha kwa wote waliokuwa wanatazama."
 
Mara ya mwisho PSG na Man City kukutana ilikuwa tarehe 4, Mei 2021.
 
City walishinda 2-0, marudiano ya nusu fainali katika uwanja wa Etihad Manchester England.
 

Takwimu za kukutana (UBINGWA WA ULAYA)

Mechi - 3
PSG - 0
City - 3
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betwa

 

Published: 09/27/2021