Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya Italia
Wiki ya 3
SSC Napoli vs Juventus FC
Estadio Diego Armando Maradona
Naples, Italia
Jumamosi, Septemba 11, 2021
SSC Napoli itamenyana na Juventus FC mechi ya
ligi kuu ya Italia katika uwanja wa Diego Armando Maradona tarehe 11 Septemba.
Napoli, kwa jina la utani Punda Wadogo walipata ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Genoa mechi ya karibuni iliyochezwa Agosti 29.
Ina maana Napoli hawajashindwa katika mechi zao 11 kwenye ligi hiyo, wakiwa wametoka sare mara tatu na kushinda mara nane.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Napoli pia hawajapoteza katika mechi 12 za nyumbani kwenye Serie A, wameandikisha ushindi mara tisa na kutoka sare mara tatu.
Wakati huo huo, Juventus walipoteza 1-0 dhidi ya Empoli wakiwa nyumbani mechi ya mwisho waliyocheza Agosti 28.
Wanajulikana kwa jina la utani kama The Old Lady, yaani Bibi Kikongwe, na hawajapata ushindi mechi mbili zilizopita- walitoka sare mara moja na kupoteza nyingine.
Hata hivyo, Juventus hawajashindwa katika mechi tano za hivi karibuni walizocheza ugenini, wakiwa wameshinda tatu mtawalia na kutoa sare mbili.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Inabidi tutie bidi katika kuwa watulivu. Haiwezekani kuwa mbele siku zote, na unapopoteza inabidi kuwa mtulivu na kuweka mambo sawa," Alisema Massimiliano Allegri, meneja wa Juventus baada ya kufungwa na Empoli.
"Mambo ni magumu kwa sasa hivi lakini tutaimarika. Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, tutakuwa na mwezi mzima katika Ligi ya Ubingwa wa Ulaya na mechi kadhaa kubwa dhidi ya wapinzani wetu na tutahitaji kujiandaa vyema.
"Tuna wachezaji kadhaa chipukizi wenye vipaji lakini wanakosa uzoefu unaohitajika kukabiliana na matukio fulani wakati wa mechi.”
Napoli na Juventus zilikutana mara ya mwisho kwenye ligi tarehe 7 Aprili 2021.
Juventus waliwafunga Napoli 2-1 katika uwanja wa Allianz.
Takwimu: (Mechi Tano Zilizopita katika Serie A)
Mechi- 5
Napoli - 2
Juventus - 3
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway