Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya England
Mechi 4 kati ya 38
Manchester United vs Newcastle United
Old Trafford
Manchester, England
Jumamosi, 11 Septemba 2021
Inaanza 17:00
Cristiano Ronaldo atakuwa kivutio kikubwa zaidi Jumamosi hii katika uwanja wa Old Trafford atakapoicheza Manchester United mechi yake ya kwanza tangu kujiunga tena na klabu hiyo, watakapowakarabisha Newcastle
ligi kuu ya England.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hatua ya Ronaldo ya kurejea tena Manchester United iligonga vichwa vya habari wiki iliyopita na atakuwa na hamu ya kuonyesha nguvu yak, huku United wakipania kuwapokonya mahasimu wao Manchester City taji la Ligi kuu msimu huu.
“Bila shaka mashabiki wamefurahia sana ndani ya siku kadhaa zilizopita, na sisi sote pia," alisema meneja wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kuhusu marejeo ya Ronaldo katika klabu hiyo. “Amefanikiwa sana katika soka, na amekuwa hapa kabla.
"Atanyanyua matumaini ya kila mtu, bila shaka. Nilicheza naye, ni mchezaji Hodari, ni binadamu wa kipekee, mchezaji mahiri, kwa hivyo ataleta msisimko mpya kwa kila mtu katika kikosi na kwa kila mtu anayehusika na klabu hii.
“Sasa hivi ana uzoefu mkubwa zaidi ya aliokuwa nao alipokuwa hapa. Amebadilika na akapata mafanikio makubwa. Kwa wanaosema eti umri wake umekwenda sana ni bora kutulia na kuacha ajionyeshe mwenyewe anachoweza kufanya," aliongeza.
United wamezoa alama saba kutokana na mechi tatu hadi kufikia sasa msimu huu nao Newcastle bado hawajashinda mechi hata moja, wamepoteza mbili na kutoa sare moja hivi karibuni kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
United walichukua alama zote sita katika mechi zao mbili dhidi Magpies msimu uliopita, wakashinda 4-1 ugenini Newcastle kisha wakawafunga 3-1 katika Old Trafford. Bruno Fernandes alifunga katika mechi zote.
Takwimu za Manchester United vs Newcastle United:
Mechi zilizochezwa: 150
Manchester United wakashinda: 76
Newcastle United wakashinda: 36
Sare: 38
Ratiba ya mechi za Ligi kuu ya England, wikendi ya 4
Jumamosi, Septemba 11
14:30 - Crystal Palace vs Tottenham Hotspur
17:00 - Watford vs Wolverhampton Wanderers
17:00 - Brentford vs Brighton & Hove Albion
17:00 - Arsenal vs Norwich City
17:00 -
Manchester United vs Newcastle United
17:00 - Southampton vs West Ham United
17:00 - Leicester City vs Manchester City
19:30 - Chelsea vs Aston Villa
Jumapili, 12 Septemba
18:30 - Leeds United vs Liverpool
Jumatatu, 13 Septemba
22:00 - Everton vs Burnley
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway