Mtanange wa miamba Chelsea na Man City


Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

2021/22 Ligi kuu ya England 

Wiki ya 6

Chelsea FC v Manchester City 

Stamford Bridge 
London, England 
Jumamosi, September 25, 2021 
Inaanza 14h30 
 
Chelsea inawakaribisha Manchester City mechi ya Ligi kuu ya England katika Stamford Bridge tarehe 25 Septemba.
 
The Blues waliwafunga mahasimu wao wa London, Tottenham Hotspurs 3-0 ugenini mechi ya karibuni Septemba 19.
 
Ni ushindi uliowapeleka kufikisha mechi tano pasipo kupoteza, wakiwa wametoka sare mara moja na kushinda mara nne.

Cesar Azpilicueta
Hakimiliki ya picha: Getty Images  

 
Chelsea pia hawajapoteza katika mechi tatu za nyumbani zilizopita kwenye Ligi Kuu ya England, wameshinda zote mtawalia.
 
"Tulipata matokeo mazuri dhidi ya timu ngumu michezo michache ya mwanzoni ," Nahodha wa Chelsea mlinzi Cesar Azpilicueta alisema baada ya ushindi dhidi ya Tottenham.
 
"Ila lazima tuwe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kujua hatuko katika kiwango bora kabisa. Timu imeonyesha tunaweza kucheza vizuri dhidi ya timu yoyote kwa njia hiyo hiyo ya kujituma, kujaribu kudhibiti mchezo, kuunda nafasi, na kucheza kama timu.
 
"Kwa sasa kazima tuendelee na bidii kwa sababu ushindi wa ligi haupatikani mwezi wa Septemba. Tuko katika nafasi nzuri lakini kazi kubwa bado iko mbele yetu.’

Gabriel Jesus
Hakimiliki ya picha: Getty Images  

 
Wakati huo huo, City walibanwa sare ya 0-0 na Southampton nyumbani mechi ya karibuni ya ligi mnamo Septemba 18.
 
Sare hiyo iliwezesha City kufikisha idadi ya mechi nne bila kupoteza kwenye ligi, wakiwa wameshinda tat una kutoa sare moja.
 
City waliwafunga Leicester City mchezo wa karibuni ugenini, ushindi uliomaliza ukame wa miezi miwili bila kupata ushindi ugenini.
 
Mara ya mwisho Chelsea na Manchester City kukutana mechi ya ligi kuu ilikuwa tarehe 8 Mei 2021.
 
Chelsea waliwalaza mabingwa watetezi City 2-1 katika uwanja wa Etihad. 
 
Takwimu (Mechi Tano Za Mwisho za Ligi)
Mechi - 5
Chelsea - 2
Man City - 3
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 09/23/2021