Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 UEFA Ubingwa wa Ulaya
Kundi E
FC Barcelona vs Bayern Munich
Camp Nou
Barcelona, Uhispania
Jumanne, 14 Septemba 2021
Inaanza 22:00
Barcelona watatazamia kudhihirisha nia yao katika
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya watakapowakaribisha Bayern Munich kwenye mechi ya kundi E jumanne jioni.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Barca wako katika hali ya kujijenga upya baada ya mshambuliaji nyota wao Lionel Messi kuondoka. Pia walimuuza Antoine Griezmann kwa Atletico Madrid wakati wa dirisha la uhamisho lakini meneja Ronald Koeman ana Imani wababe hao wa Uhispania wataendelea kuwa washindani msimu huu.
Wachezaji wapya waliosajiliwa- Memphis Depay, Sergio Aguero, Eric Garcia na Luuk de Jong wanaipa sura mpya Barcelona.
"Siku zote kuna mambo ya kuimarisha lakini nitakwambia kitu kimoja: kila mmoja akiwepo tunaweza kufanya mambo makubwa,’’ alisema Koeman kuhusu uwezekano wa Barcelona msimu huu.
"Tuna timu nzuri. Lakini bado lazima tuwe wakweli, itakuwa vigumu, ila nina Imani na matarajio,’’
Bayern wako chini ya uongozi mpya wa meneja Julian Nagelsmann aliyechukua mikoba kutoka kwa meneja mpya wa Ujerumani Hansi Flick mwanzoni mwa msimu. Dayot Upamecano na Marcel Sabitzer wamemfuata kujiunga na mabingwa hao mara sira wa ulaya, wakitokea RB Leipzig ambayo waliifunga 4-1 katika Bundesliga Jumamosi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hii itakuwa mara ya kwanza timu hizi mbili kukutana tangu ushindi mkubwa wa Bayern wa 8-2 dhidi ya Barcelona mwaka uliopita. Mabingwa hao wa Ujerumani walishinda ubingwa wa ulaya msimu huo, huku Lewandowski ambaye ni wa tatu katika rekodi ya wafungaji bora wa ligi ya ubingwa wa ulaya akiwabeba.
Takwimu za FC Barcelona vs Bayern Munich:
Mechi :9
FC Barcelona wakashinda: 3
Bayern Munich wakashinda: 5
Sare: 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway