Milan yalenga kuendeleza mwanzo mzuri Serie A


Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

2021/22 Ligi kuu ya Italia

Wiki ya 6 kati ya 38

Spezia vs AC Milan  

Stadio Alberto Picco
La Spezia, Italia
Jumamosi, 25 Septemba 2021
Itaanza 16:00 
 
AC Milan watakuwa wanalenga kuendeleza mwanzo mzuri ambao wamekuwa nao msimu huu wa 2021/22 Ligi kuu ya Italia Serie A watakapocheza dhdi ya Spezia Jumamosi alasiri.

Stefano Pioli
Hakimiliki ya picha: Getty Images  

 
AC Milan wanaingia wikendi wakiwa nguvu saw ana mahasimu wao wa nyumbani na mabingwa watetezi Inter Milan, kwa alama 13, baada ya kushinda mechi nne kati ya tano msimu huu.
 
Milan walilazimika kuongeza bidi katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Venezia mapema wiki hii lakini meneja Stefano Pioli amefurahishwa na hatua ambazo timu yake imepiga ndani ya miaka miwili.
 
“Nilijua kazi tuliyofanya msimu uliopita italipa msimu huu, ni mchakato na lazima tungefikia viwango hivi tu," Pioli aliambia DAZN baada ya matoke ohayo.  
 
“Tulishinda michezo mingi msimu uliopita, lakini kwa maoni yangu kitu muhimu ambacho tunacho sasa ni ukomavu na pia unngwaji mkono kutoka mashabiki, mambo ambayo msimu uliopita yalikosekana. Lengo letu ni kuimarisha rekodi ya nyumbani kutoka msimu uliopita, na nadhani tunaweza kufanya hivyo kwa msaada wa mashabiki wetu katika San Siro," aliongeza. 
 
Spezia walikuwa wanaongoza 2-1 dhidi ya Juventus ugenini siku ya Jumatano jioni lakini hatimaye wakaishia kufungwa 3-2 na kumaliza simu wakiwa kwenye nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi.

Thiago Motta
Hakimiliki ya picha: Getty Images  

 
Msimu uliopita, timu hizi mbili ziligawana alama zilipokutana mara mbili. Milan walishinda 3-0 katika uwanja wa San Siro kabla ya kufungwa 2-0 na Spezia nyumbani.
 

Takwimu za Spezia vs AC Milan:

 

Mechi zilizochezwa 3
Spezia wakashinda: 1
AC Milan wakashinda 2
Draws: 0
 

Ratiba ya Serie A matchday 6:  

 
Jumamosi, 25 Septemba 
 
16:00 - Spezia vs AC Milan 
19:00 - Inter vs Atalanta 
21:45 - Genoa vs Verona 
 
Jumapili, 26 Septemba 
 
13:30 - Juventus vs Sampdoria 
16:00 - Udinese vs Fiorentina 
16:00 - Sassuolo vs Salernitana
16:00 - Empoli vs Bologna 
19:00 - Lazio vs Roma 
21:45 - Napoli vs Cagliari 
 
Jumatatu, 27 Septemba 
21:45 - Venezia vs Torino 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 09/24/2021