Medvedev atafuta fainali ya pili US Open


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021 US Open 

Mashindano ya Tennis ya Grand Slam 

USTA Billie Jean King National Tennis Center
New York City, New York, Marekani 
10-12 Septemba 2021
 
Mrusi Daniil Medvedev atakuwa anatafuta kufika fainali ya mashindano ya Tenis ya US Open kwa mara ya pili katika fani yake mwaka huu.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kuchuana dhidi ya FĂ©lix Auger-Aliassime wa Canada kwenye fainali September 10 saa  22h00.
 
Medvedev alifika nusu fainali kwa mara ya tatu mtawalia kwenye mashindano ya US Open baada ya kumshinda Mholanzi Botic van de Zandschulp kwenye robo fainali tarehe 7 Septemba.

Felix Auger-Aliassime
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
“Atakayeshinda lazima atakuwa amewaka moto. Unajua wana umri mdogo zaidi yangu. Mimi si mzee,” Medvedev alisema kuhusu kukutana na  Auger-Aliassime mwenye umri wa miaka 21.
 
"Lakini kwake ni nusu fainali ya kwanza ya mashindano makubwa ya Grand Slam. Uzoefu sio kila kitu, kwa sababu nilipocheza nusu fainali kwa mara ya kwanza katika Grand Slam nilishinda.
 
"Haimaanishi unapocheza nusu fainali kwa mara ya kwanza utapoteza. Lakini nafurahia kuwa na uzoefu huo. Najua ikoje. Sitakuwa mwoga. Najua hivyo.”
 
Mchezaji huyo ambaye makao yake ni Monaco kwa sasa anaorodheshwa nambari mbili duniani na chama cha wacheza Tennis wa kulipwa (ATP) lakini hajawahi kushinda Grand Slam hata moja.
 
Novak Djokovic
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Medvedev alimaliza wa pili kwenye mashindano ya US Open mwaka wa 2019, na pia kwenye mashindano ya 2021 Australia Open, ambapo alishindwa na Mwispania Rafael Nadal na gwiji wa mchezo huo Mserbia Novak Djokovic. 
 
Kama mchezaji aliyeorodheshwa wa tatu kwenye mashindano ya US Open, Medvedev alifika nusu fainali bila kupoteza seti hata moja kabla ya hatimaye kushindwa na Dominic Thiem aliyeibuka bingwa.
 
Hii itakuwa mara ya pili Medvedev na Auger-Aliassime kukutana katika mashindano.
 
Medvedev alimshinda Auger-Aliassime 3-6, 6-4, 7-6(9) katika mechi ya raundi ya pili kwenye mashindano ya Rogers Cup  2018.
 
Mshindi kati ya Medvedev na Auger-Aliassime atakutana na  Djokovic au Alexander Zverev kwenye fainali ya 2021 US Open mnamo Septemba 12.
 

Mashindano ya US Open 2020 fainali ya wanaume

Dominic Thiem alimshinda Alexander Zverev
 

Mashindano ya US Open 2020 fainali ya wanawake 

Naomi Osaka alimshinda Victoria Azarenka 
 

Bashiri tenisi mtandaoni

Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 09/10/2021