Man Utd na Leeds kurejesha uhasama msimu wa 2021/22


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021-22 Ligi kuu ya England

Mechi 1 kati ya 38

Manchester United vs Leeds United 

Old Trafford 
Manchester, England
Jumamosi, Agosti 14, 2021
Mechi inaanza 14:30 
 
Manchester United na Leeds zitarejelea upya uhasama baina yao timu hizo zitakapokutana katika mechi ya ufunguzi wa msimu wa 2021/22 ligi kuu ya England Jumamosi hii.
 
Manchester United midfielder Bruno Fernandes
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

Manchester United ambao msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya Manchester City, safari hii wamesajili wachezaji wapya Jadon Sancho na Raphael Varane katika jaribio la kuwazidi nguvu mahasimu wao wa nyumbani.
 
United walimaliza alama 12 nyuma ya City na wakalipa gharama ya kutetereka mwanzoni mwa msimu, tatizo ambalo meneja Ole Gunnar Solskjaer anatumai watajirekebisha msimu huu.
 
"Pep (Guardiola)alisema 'Huwezi kushinda ligi katika mechi nane za kwanza za msimu, lakini unaweza kupoteza fursa ya kushinda ligi,’na ndicho kilichotokea msimu uliopita, “ amesema Solskjaer.

"Ni bora kujiamini na kukosea kuliko kujishuku na ikawa hivyo. Bila shaka vijana hawa wanaweza kushinda ligi wakijituma kikamilifu na kujitolea.”

"Nahisi ni kama msimu unaokuja utakuwa kati ya misimu yenye nguvu zaidi katika ligi kuu ya England.”
 
"Kwa muda sasa umekuwa mpambano kati ya Manchester City na Liperpool, lakini sisi na Chelsea tumetumia hela nyingi kusajili wachezaji wapya na tutakuwa kwenye kinyang’anyiro, “ aliongeza.
 
Leeds walijituma vilivyo wakiwa wanarejea katika ligi kuu ya England baada ya miaka mingi, wakamaliza kwenye nafasi ya 9 kufuatia ushindi wa mechi nne mfululizo kuelekea mwisho wa msimu wa 2021/21.
 
Marcelo Bielsa amefanikiwa kubakisha wachezaji wote wa kutegemewa, akamsajili Junior Firpo na pia klabu ikampa mkataba wa kudumu Jack Harrison- na kwa hivyo wana uwezekano wa kupata matokeo bora zaidi msimu huu.
 
Mshambuliaji wa Leeds United Patrick Bamford
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

Manchester United walishinda mechi ya nyumbani 6-2 katika Old Trafford na ugenini Leeds mechi ikamalizika 0-0.
 

Takwimu za michuano kati ya Manchester United na Leeds:


Mechi zilizochezwa: 91
Manchester United wakashinda: 37
Leeds United wakashinda: 23
Sare: 31
 

English Premier League fixtures, matchday 1


Mechi za Ligi kuu ya England, siku ya 1
 
Ijumaa, 13 Agosti 2021
 
22:00 - Brentford vs Arsenal 
 
Jumamosi, 14 Agosti 2021
 
14:30 - Manchester United vs Leeds United
17:00 - Leicester City vs Wolverhampton Wanderers 
17:00 - Chelsea vs Crystal Palace 
17:00 - Watford vs Aston Villa 
17:00 - Everton vs Southampton 
17:00 - Burnley vs Brighton & Hove Albion
19:30 - Norwich City vs Liverpool 
 
Jumapili, 15 Agosti 2021
 
16:00 - Newcastle United vs West Ham United 
18:30 - Tottenham Hotspur vs Manchester City 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

 

Published: 08/10/2021