Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya England
Mechi ya 2 kati ya 38
Southampton vs Manchester United
Uwanja wa St Mary's
Southampton, England
Jumapili, Agosti 22 2021
Manchester United wanatazamia kuendeleza mwanzo wao mzuri wa msimu wa
2021/22 wa Ligi kuu ya England watakapokutana na Southampton Jumapili.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Southampton walianza kampeni kwa kupoteza 3-1 dhidi ya Everton. Adam Armstrong aliwafungia goli lao mapema wakawa wanaongoza uwanjani Goodison Park lakini Everton wakafunga matatu na kuondoka na alama zote tatu.
Upande wao, Manchester United waliwafunga Leeds 5-1 huku Bruno Fernandes akifunga goli tatu, naye Pogba akisaidia mara nne upatikanaji wa magoli.
"Watu huzungumzia sifa za Paul [(Pogba), lakini sifa zake haziko katika mazungumzo,” alisema Fernandes kufuatia mchezo wa kufana waliouonyesha uwanjani Old Trafford mwishoni mwa wiki iliyopita. "Tunajua anachoweza kufanya na leo ameonyesha hivyo. Ni mchezaji muhimu sana kwetu.”
"Tunajua uwezo wa wachezaji ambao wamejiunga, lakini timu tayari ilikuwa nzuri sana, tulionyesha msimu uliopita,” aliongeza Fernandes. "Hatukushinda mataji, lakini timu iliendelea kukua. Kwa fikira hiyo tutafanikiwa.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Msimu uliopita United waliwafunga Southampton 3-2 katika uwanja wa St Mary's kabla ya kuwanyeshea 9-0 mechi ya marudiano katika Old Trafford.
Takwimu za Southampton vs Manchester United:
Mechi zilizochezwa: 92
Southampton wakashinda: 17
Manchester United wakashinda: 52
Sare: 23
Ratiba ya mechi za Ligi kuu ya England, wiki ya 2
Jumamosi, 21 Agosti 2021
13:30 - Liverpool vs Burnley
16:00 - Aston Villa vs Newcastle United
16:00 - Crystal Palace vs Brentford
16:00 - Leeds United vs Everton
16:00 - Manchester City vs Norwich City
18:30 - Brighton & Hove Albion vs Watford
Jumapili, 22 Agosti 2021
15:00 - Southampton vs Manchester United
15:00 - Wolverhampton Wanderers vs Tottenham Hotspur
17:30 - Arsenal vs Chelsea
Jumatatu, 23 Agosti 2021
21:00 - West Ham United vs Leicester City
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway