Mambo Tayari kwa Ryder Cup 2021


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021 Ryder Cup 

Mashindano ya Golf

Marekani vs Ulaya 

Whistling Straits
Haven, Wisconsin, Marekani 
24-26 Septemba 2021
 
Michuano ya Mashindano ya Golf ya Ryder Cup Mzitafanyika katika uwanja wa Straits, Whistling Straits, Haven, Wisconsin, Marekani kati ya tarehe 24 na 26 Septemba.
 
Shindano hilo hukutanisha timu ya Marekani na timu ya Ulaya kila baada ya miaka miwili,  lakini yaliahirishwa mwaka 2020 kutokana na janga la Covid-19.
 
Timu ya Ulaya ndiyo inayoshikilia taji la Ryder Cup kwa sasa baada ya ushindi wa 17½–10½ dhidi ya Marekani 2018 katika uwanja wa Le Golf National eneo la Guyancourt, kusini magharibi mwa Paris, Ufaransa.
 
Huku kukiwa na alama 28 za kushindaniwa, alama 14½ zinahitajika kushinda kombe hilo, na pia mabingwa watetezi Timu ya Ulaya wanahitaji alama 14 kutetea kombe.

Dustin Johnson
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Nahodha wa timu ya Marekani Steve Stricker amejumuisha majina mashuhuri kama Daniel Berger, Harris English, Tony Finau, Xander Schauffele, Scottie Scheffler na Jordan Spieth katika kikosi chake cha wachezaji 12.
 
Nao Collin Morikawa, Dustin Johnson, Bryson DeChambeau, Brooks Koepka, Justin Thomas na Patrick Cantlay walifuzu kushiriki kufutia matokeo katika mashindano ya PGA Tour’s BMW.
 
Kwa upoande mwingine, Nahodha wa Timu ya Ulaya Padraig Harrington amewajumuisha  Sergio Garcia, Shane Lowry na Ian Poulter kukamilisha timu yake ya wachezaji 12.
 
Wachezaji hao watatu wanaungana na wale waliofuzu moja kwa moja, ambao ni: Paul Casey, Matt Fitzpatrick, Tommy Fleetwood, Tyrrell Hatton, Viktor Hovland, Rory McIlroy, Jon Rahm, Lee Westwood na Bernd Wiesberger.

Sergio Garcia
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
"Nitasema kuna msisimko wa kiwango cha juu," alisema Mkurugenzi wa mashindano ya  Ryder Cup Jason Mengel kabla ya mashindano kuanza.
 
 "Namaanisha tumesimama hapa, ikiwa ni chici ya wiki tatu kabla ya kuwakaribisha mashabiki wa golf kutoka kote duniani.
 
"Na wachezaji walio bora zaidi kutoka Marekani na wachezaji bora kutoka Ulaya, kuja hapa  Wisconsin katika uwanja wa Whistling Straits," aliongeza.
 
"Kohler alituzwa na Wisconsin alituzwa Ryder Cup mwaka wa 2005. Tuna matarajio makubwa sana safari hii."
 

Washindi wa Ryder Cup miaka mitano iliyopita

2010 - Ulaya
2012 - Ulaya 
2014 - Ulaya
2016 - Marekani 
2018 - Ulaya
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/21/2021