Macho yote kwa British MotoGP 2021


Hakimiliki ya picha: Getty Images

Ubingwa wa Dunia wa MotoGP 2021

British MotoGP 

Awamu ya 12
Silverstone Circuit
Silverstone, England 
Jumapili, 29 Agosti 2021
  
Mashindano ya mbio za pikipiki ya British MotoGP 2021 ambayo pia yanajulikana kama Monster Energy British Grand Prix yatafanyika eneo la Silverstone, England mnamo tarehe 29 Agosti.
  
Yatakuwa awamu ya 12 ya ubingwa wa dunia wa mashindano ya pikipiki na yamepangiwa kufanyika katika uwanja wa Silverstone.  
  
Mashindano ya British MotoGP yanarejea baada ya kufutwa mwaka uliopita kutokana na janga la Covid-19.
  
Mashindano ya mara ya mwisho yalifanyika 2019 na mshindi alikuwa Alex Rins wa timu ya Suzuki, akifuatwa na Marc Marquez wa timu ya Honda naye mwendeshaji wa timu ya Yamaha Maverick Vinales akamaliza wa tatu.
  
Fabian Quartararo of Yamaha (Fabian Quartararo wa Yamaha)
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
Mashindano ya hivi karibuni katika ubingwa wa dunia wa mbio za pikipiki- MotoGP msimu wa 2021 yalikuwa ya Austrian MotoGP yaliyofanyika Agosti 15.
  
Mshindi kwenye mashindano hayo ya kuchangamsha alikuwa Brad Binder wa timu ya KTM akifuatwa na waendeshaji wawili wa timu ya Ducati Francesco Bagnaia na Jorge Martin, kwenye nafasi ya pili na ya tatu.
  
Mwendeshaji wa Yamaha Fabio Quartararo bado anaongoza kwenye msimamo wa 2021 wa waendeshaji baada ya kujikusanyia alama 181 huku pambano la taji la dunia la MotoGP likizidi kupamba moto.
  
Bagnaia (alama 134) na mwendeshaji wa Suzuki Joan Mir (alama 134) sasa wako kwenye nafasi ya pili na tatu kwa utaratibu huo.
  
Joan Mir of Suzuki
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
"Nina furaha kubwa ya kuondoka na ushindi leo,” Binder alisema baada ya kutwaa ushindi kwa mara ya kwanza msimu huu, uliomuweka kwenye nafasi ya sita akiwa na alama 98.
  
“mwanzo wa shindano ulikuwa mgumu sana kwetu. Kwa bahati mbaya nilipata gurudumu baya zaidi kuwahi kutokea tangu nilipoanza. Kwa hivyo nilikuwa napata ugumu sana kwenye maeneo ya kupiga breki kwa kutumia kithibiti.
  
"Lakini nilipoona mvua ikianza, nilichukua nafasi yangu na kupambana kwa bidii niwezavyo nikapunguza umbali uliokuwepo na kundi la mbele, na lilikuwa jambo zuri.”
  
Katika msimamo wa timu, Ducati wanaongoza wakifuatwa na Yamaha kwenye nafasi ya pili, nao KTM wako katika nafasi ya tatu.
  

Matokeo ya British MotoGP 2019


Mshindi: Alex Rins - Suzuki 
Mshindi wa pili: Marc Marquez - Honda 
Nafasi ya tatu: Maverick Vinales - Yamaha 

Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsportmpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

 

Published: 08/25/2021