Kipute kingine cha Wababe Liverpool na Man City


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Ligi kuu ya England

Mechi ya 7 kati ya 38

Liverpool vs Manchester City 

Anfield 
Liverpool, England
Jumapili, 03 October 2021
Kick-off is at 18:30 
 
Liverpool na mabingwa watetezi Manchester City watakutana tena katika mtanane mwingine wa ligi kuu ya England msimu huu wa 2021/22 katika uwanja wa Anfield siku ya Jumapili.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Bado ni mapema katika msimu, lakini mechi hiyo huenda ikaweka msingi wa nani ataibuka bingwa wa ligi katika msimu ambao tayari umedhihirika una ushindani mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
 
Liverpool ndio timu pekee kwenye ligi hiyo ambayo haijapata kushindwa msimu hu una wanaingia katika mechi ya saba wakiwa wanaongoza kileleni- wakiwazidi City kwa alama moja na timu zingine nne, baada ya kutoka sare 3-3 na Brentford walipandishwa msimu huu.
 
"Walistahili magoli hayo matatu. Nadhani tungeweza kufunga mengi zaidi; wangeweza kufunga moja zaidi, tungeweza kufunga zingine nne au tano na ingependeza zaidi. Lakini ni sawa, tuliondoka na alama moja, na wao moja, sasa tusonge mbele," Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kufuatia mechi hiyo dhidi ya Brentford.  
 
Pep Guardiola alivikwa kofia ya meneja wa City aliyefanikiwa zaidi kwa idadi ya mechi walizoshinda wakati walipowafunga mabingwa wa Ulaya Chelsea 1-0.
 
"Najivunia. Tumefanikiwa katika Stamforf Bridge dhidi ya mabingwa wa Ulaya. Tulikuwa kikosi imara kabisa. Inanipa raha , mimi mwenyewe lakini zaidi kwa klabu," Guardiola aliambia waandishi baada ya mechi hiyo.
 
"Leo hawa wachezaji walikuwa katika kiwango kingine. Katika uwanja huu, na dhidi ya wapinzani, kuweza kufanya hivyo hunipa furaha sana. Tunaposhinda, meneja ni hodari, tunaposhindwa inakuwa sivyo. Naelewa kila kitu."
 
Mohamed Salah
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Msimu uliopita, City walizoa alama nne kutoka Liverpool. Baada ya kutoka sare 1-1 katika Etihad waliwafuata Liverpool nyumbani Anfield na kuwazaba 4-1, huku Mohamed Salah akifunga penalti katika mechi zote mbili.
 

Takwimu za Liverpool vs Manchester:

 
Idadi ya Mechi: 170
Liverpool wakashinda: 80
Manchester City wakashinda: 47
Sare: 43
 

Ratiba ya mechi za Ligi Kuu ya England, wiki ya 7

 
Jumamosi, 02 Octoba 
 
13:30 - Manchester United vs Everton
16:00 - Chelsea vs Southampton 
16:00 - Wolves vs Newcastle United
16:00 - Burnley vs Norwich City 
16:00 - Leeds United vs Watford 
18:30 - Brighton & Hove Albion vs Arsenal 
 
Jumapili, 03 Octoba 
 
15:00 - Tottenham Hotspur vs Aston Villa 
15:00 - West Ham United vs Brentford 
15:00 - Crystal Palace vs Leicester City 
17:30 - Liverpool vs Manchester City 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betwa
 

Published: 09/29/2021