Juventus yamulika ushindi wa kwanza katika Serie A


Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

2021/22 Serie A 

Wiki ya 5 of 38

Spezia vs Juventus  

Stadio Alberto Picco
La Spezia, Italia 
Jumatano, 22 Septemba 2021
Inaanza 19:30 

Juventus watakuwa wanatafuta ushindi wa kwanza kabisa katika msimu huu wa 2021/22 wa Ligi kuu ya Italia- Serie A jumatano jioni.

Massimiliano Allegri
Hakimiliki ya picha: Getty Images  

 
Juve wamekuwa na mwanzo mbaya wa msimu, na hawajashinda bado baada ya kucheza mechi nne. Walitoka sare 2-2 dhidi ya Udinese ugenini mechi ya kufungua msimu kabla ya kufungwa na Empoli na Napoli.
 
Baada ya kufungwa na Napoli, walitoka sare na AC Milan mwishoni mwa wiki iliyopita, na wanaonekana kupungukiwa na makali baada ya Christiano Ronaldo kuondoka kurejea Manchester United.
 
"Lazima ujitume, ili kuweza kukaba vizuri. ndio mchakato wa kukua kwa wachezaji,” alisema meneja wa Juve Massimiliano Allegri kufuatia matokeo ya Jumapili.  

"Nakiri nilifanya makosa katika kupumzisha wachezaji, nilikosea. Ningetakiwa kuingiza wachezaji wenye uwezo wa kulinda ili kuhakikisha tunakaa na uongozi wa 1-0, kwa hivyo nakubali makosa.”
 
Mwanzo huo mbaya umewaacha Juventus eneo la kushushwa daraja, wakiwa alama mbili tu nyuma ya Spezia walioandikisha ushindi wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Venezia ugenini siku ya Jumapili.

Thiago Motta
Hakimiliki ya picha: Getty Images  


Msimu uliopita, Juventus walizoa alama sita kutoka Spezia. Walifuatisha ushindi wa 4-1 ugenini na mwingine wa 3-0 nyumbani Turin. Alvaro Morata alifunga katika mechi zote mbili.
 

Takwimu za Spezia vs Juventus :


Idadi ya Mechi: 4
Spezia wakashinda: 1
Juventus wakashinda: 2
Sare: 1

Ratiba ya Mechi za Serie A, wiki ya 5:  

 
Jumanne, Septemba 21 
 
19:30 - Bologna vs Genoa 
21:45 - Fiorentina vs Inter 
21:45 - Atalanta vs Sassuolo 
 
Jumatano, Septemba 22 
 
19:30 - Spezia vs Juventus 
19:30 - Salernitana vs Verona 
21:45 - Milan vs Venezia 
21:45 - Cagliari vs Empoli 
 
Alhamisi, 23 Septemba
 
19:30 - Sampdoria vs Napoli 
19:30 - Torino vs Lazio 
21:45 - Roma vs Udinese 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/21/2021