Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya Italia-Serie A
Matchday 2
Juventus FC v Empoli FC
Allianz Stadium
Torino, Italia
Jumamosi, 28 Agosti 2021
Inaanza 21H45
Juventus FC itacheza dhidi ya Empoli kwenye ligi kuu ya Italia- Serie A katika uwanja wa Allianz mnamo Agosti 28.
Juve ambao jina lao la utani nyumbani ni ‘The Old Lady’ yaani bibi kikongwe, walitoka sare 2-2 dhidi ya Udinese ugenini mechi iliyopita iliyochezwa Agosti 22.
Sare hiyo iliwapeleka Juventus kufikisha mechi nne mtawalia bila kupoteza katika ligi hiyo, kufuatia sare nyingine moja na ushindi wa mechi tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Juventus pia wameshinda mechi tatu kati ya nne walizocheza ugenini katika Serie A, na nyingine wakafungwa na AC Milan.
Massimiliano Allegri, meneja wa Juventus, alielezea kilichokwenda mrama katika kikosi chake kufuatia sare dhidi ya Udinese.
“Tulicheza vizuri, lakini katika mpira wa miguu jambo la muhimu zaidi ni kushinda na kujua jinsi ya kuisoma mechi. Katika nusu ya pili, tulipoteza mipira miwili, mitatu, au mingi sana katikati,” Allegri alisema.
"Labda pia ni kutokana na joto na hali mwanzoni mwa msimu. Kwa hali yoyote, huwezi kufungwa goli kama lile, hususan ikiwa hakukuwa na mpira wowote uliolenga lango lako kabla kama ilivyotokea usiku huu.
"Tunapoupata mpira, kwa sababu ya sifa za wachezaji, inabidi haraka tuidhibiti nafasi: na tulifanya hivyo jioni hii.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Wakati huo huo, Empoli walifungwa 3-1 na Lazio nyumbani mechi yao iliyopita mnamo Agosti 21.
Matoke hayo yana maana Empoli hawajapata ushindi katika mechi mbili zilizopita katika ligi hii, wakiwa wamepoteza mbili mfululizo.
Empoli pia wamepoteza mechi mbili kati ya tatu walizocheza ugenini katika Serie A, na mechi nyingine moja wakawafunga Sampdoria.
Mara ya mwisho Juventus na Empoli kukutana mchezo wa ligi ilikuwa tarehe 30 Machi, 2021.
Juventus walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Empoli katika uwanja wa Allianz.
Takwimu (Mechi tano za Serie A karibuni)
Mechi - 5
Juventus - 5
Empoli - 0
Sare- 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway