Joshua ataka ‘kumuenzi McCracken kwa ushindi’


Hakimiliki ya picha: Getty Images


Anthony Joshua v Oleksandr Usyk

WBA (Super), IBF, WBO na and IBO Heavyweight Ubingwa wa Dunia

Septemba 25, 2021
Tottenham Hotspur Stadium, London
 
Bondoa Anthony Joshua anatazamia kutwaa ushindi kwa heshima ya kocha wake Rob McCracken atakapopigana na Oleksandr Usyk kutetea mataji yake ya ubingwa wa dunia wa WBA (Super), IBF, WBO na IBO Heavyweight Jumamosi tarehe 25 Septemba 2021 katika uwanja wa Tottenham Hotspur Stadium mjini London.
 
Joshua (24-1, 22 KO) anaingia katika pigano hilo baada kumshinda Kubrat Puley aliyemwangusha katika raundi ya tisa mwezi Disemba mwaka uliopita, huku naye Usyk (18-0, 13 KO) mara ya miwsho alipigana na Oktoba 2020 akamshinda Mwingereza Derik Chisora kupitia baada ya raundi 12.

Oleksandr Usyk
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Joshua alianza kambi ya mazoezi kwa ajili ya pigano hili bila kocha wake wa miaka mingi  McCracken, ambaye alikuwa amesafiri na timu ya Uingereza kwenye michezo ya Olimpiki mjini Tokyo, Japana. 
“Bilas haka Rob ni kiongozi wa ajabu. Awepo, asiwepo, unahisi kama yupo tu,” alisema bondia huyo mwenye miaka 31. 
 
“Lakini kwa namna Fulani ilienda vizuri kwa sababu tuna timu nzuri. Siku zote naangalia mazoezi ya kizamani- Manny Pacquiao alikuwa na Freddie Roach kama mwalimu. Kevin Rooney, Teddy Atlas na Cus D'Amato walimfunza Mike Tyson]. Mabondia wengine huhamia kwa waalimu tofauti.”

Rob McCracken
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Joshua aliwaongeza Angel Fernandez na Joby Clayton katika kikosi chake cha mazoezi baada ya kupigwa na Andy Ruiz Jr lakini, wakati wote huo Imani yake katika McCracken ikaongezeka maradufu.
 
Bingwa huyo wa uzani wa Heavy alisema kuhusu McCracken: "Lazima nishinde pigano kwa ajili ya Rob. Inabidi nipigane kwa ajili ya Rob.” Aliongeza: “Kocha anaweza kutumia mfumo ule ule lakini inabidi aelewe mabondia tofauti hufanikiwa kwa mbinu gani. Huenda nikahitaji kutiwa moyo zaidi: ‘ Jamani, jitume kabisa kwa ajili ya Watoto wako!' Unaweza kuhitaji kusikia- 'Ongeza bidi, tunakwenda hadi raundi 20!'”
 

Taarifa za Mabondia hao

Anthony Joshua
Jina la Utani: AJ
Uraia: Muingereza
Umri: 31
Rekodi: 24-1 (22 KO)
Urefu: 198cm
Reach: 208cm
Stance: Orthodox
- Bingwa wa Dunia wa WBA (Super), IBF, WBO na IBO 
- Mshindi wa Dhahabu Olimpiki 2012, Super-heavyweight
 
Oleksandr Usyk
Jina la Utani: The Cat
Uraia: Ukrain
Umri: 34
Rekodi: 18-0 (13 KO)
Urefu: 191cm
Reach: 198cm
Stance: Southpaw
- Mshindi wa Dhahabu Olimpiki 2012, Heavyweight
- WBO mandatory challenger

 

Bashiri ndondi na Betway


Tunakuletea mapambano bora ya ndondi na unaweza kubashiri kwa kutumia simu au kompyuta yako. Weka ubashiri wako kwa urahisi na uwashangilie mabondia unaowapenda kiganjani mwako. Betway inakupa kile unachotaka kwenye Ulimwengu wa kubashiri ndondi live. Rusha ngumi na ingia ulingoni nasi tunakupa odds nono. Bashiri kwenye mapambano makubwa na Betway Tanzania.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/23/2021