Cadiz Yajitapa Itakomesha Barcelona


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Ligi Kuu Ya Uhispania

Wiki ya 6 

Cadiz CF v FC Barcelona 

Estadio Nuevo Mirandilla 
Cádiz, Uhispania
Alhamisi, 23 Septemba 2021 
Inaanza 23h00 
 
Cadiz CF itapimana nguvu na FC Barcelona mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La liga, katika uwanja wa Ramón de Carranza Stadium tarehe 23 Septemba.
 
Cadiz, wajulikanao kama nyambizi ya njano, walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Celta Vigo mechi ya mwisho waliyocheza, na ilikuwa ugenini tarehe 17 Septemba.
 
Matokeo hayo yalimaliza mfululizo wa mechi saba bila ushindi kwa Cadiz katika ligi hiyo, wakiwa wameshindwa mara nne na kutoka sare mara tatu.
 
Anthony Lozano
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Hata hivyo, Cadiz wamekosa ushindi katika mechi nne walizocheza nyumbani karibuni katika La Liga, wakapoteza tatu na kutoa sare moja.
 
Wakti huo huo, Barcelona walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Getafe wakichezea nyumbani mechi ya karibuni Agosti 29, na watawakaribisha Granada Agosti 20.
 
Ushindi dhidi ya Getafe uliwawezesha Barcelona kufikisha mechi nne mfululizo bila kupoteza katika ligi hiyo wakiwa wameshinda mara tatu na kutoka sare mara moja.
 
Barcelona wanaona fahari ya kutopoteza katika mechi tano za ugenini mtawalia, wakiwa wameshinda tatu na kutoka sare mara mbili.  

Ronald Koeman
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
"Tuna uwezo wa kushinda kila mechi. inabidi tujiandae vizuri, hata hivyo, na kuimarisha ulinzi," Meneja wa Barcelona Ronald Koeman alisema kabla ya mtanange wao dhidi ya Granada na Cadiz.
 
"Kuna mifumo mbali mbali unaweza kutumia kushinda mechi, na timu nyingi zinayo. Inategemea wachezaji. Mfumo wa msingi ni ule wa 4-3-3 
 
"Lakini inategemea una washambuliaji wangapi au idadi ya walinzi ulio nao. Kama tungecheza mchezo wa wazi zaidi dhidi ya Bayern (Munich), tungefungwa magoli mengi zaidi.”
 
Mechi ya mwisho ya ligi kati ya Cadiz na Barcelona ilikuwa Februari 21 2021.
 
Iliishia kwa sare ya 1-1 katika uwanja wa Camp Nou.
 

Takwimu: (Mechi Nne Zilizopita)

Mechi - 4
Cadiz - 1
Barcelona - 2
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 09/21/2021