Atletico kukaribisha Bilbao


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Ligi Kuu ya Uhispania

Siku ya 5

Atletico Madrid v Athletic Bilbao 

Estadio Wanda Metropolitano 
Madrid, Uhispania
Jumamosi, 18 Septemba 2021
Inaanza 17h15 

Atletico Madrid itakutana na Athletic Bilbao kwenye Ligi kuu ya Uhispania- La Liga, katika uwanja wa Estadio Wanda Metropolitano Septemba 18.  
 
Watengeneza magodoro hao walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Espanyol ugenini mechi ya mwisho iliyochezwa Septemba 12.
 
Ushindi huo umeongeza idadi ya mechi walizocheza Atletico bila kupoteza kufikia tisa, wakiwa wameshinda saba na kutoa sare mbili.

Yannick Carrasco
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Pia hawajapoteza katika mechi tisa za nyumbani walizocheza karibuni kwenye La Liga, wakiwa wameandikisha sare mbili na kushinda mechi saba mtawalia.
 
Wakati huo huo, Bilbao walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Mallorca mechi ya mwisho waliyocheza mnamo tarehe 11 Septemba.
 
Ushindi huo uliwapeleka kufikisha idadi ya mechi nne bila kupoteza katika ligi hiyo wakiwa wameandikisha sare mbili mtawalia na ushindi wa mechi mbili mfululizo.
 
Bilbao pia hawajapoteza mechi mbili za ugenini walizocheza karibuni kwenye La Liga- wameshinda moja na kutoka sare nyingine.

Marcelino
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
“Tumezoa alama nane kutoka kwa 12. Inabidi tunyenyekee na kuwaheshimu wapinzani wetu. Tuna furaha,’’ alisema meneja wa Bilbao Marcelino Garcia Torel baada ya mechi yao dhidi ya Mallorca.
 
 
"Tuendelee kutumainia tunaweza kushinda mechi zingine. Tumeimarika katika maeneo mengi ya mchezo ukilinganisha na msimu uliopita. Timu hii, inavyocheza, inahusisha watu.
‘’
 
“Mwaka uliopita tulifungwa magoli machache sana, lakini makosa ya hapa na pale yalituangusha. Wapinzani wetu wanajitengenezea nafasi za kufunga kutokana na uwezo wao, sio kutokana na udhaifu wetu. Na hivyo ni vizuri.”
 
Mara ya mwisho Atletico na Bilbao zilipokutana ilikuwa mnamo Aprili 25, 2021.
 
Atletico walipata ushindi wa 2- 1 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Estadio Wanda Metropolitano. 
 

Takwimu (Mechi Tano za La Liga zilizopita)

Mechi - 5
Atletico - 3
Bilbao - 1
Sare- 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/14/2021