Atletico, Barcelona kumenyana La Liga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Ligi kuu ya Uhispania

Wiki ya 8

Atletico Madrid v FC Barcelona

Estadio Wanda Metropolitano 
Madrid, Uhispania
Jumamosi, 02 Octoba 2021
Kuanzia 22h00 

Atletico Madrid itakutana na FC Barcelona kwenye Ligi kuu ya Uhispania- La Liga katika uwanja wa Estadio Wanda Metropolitano jumamopsi Octoba 02. 
 
Atletico au watengeza magodoro walicharazwa 1-0 na Alaves ugenini mechi yao ya karibuni katika ligi, mnamo Septemba 25.
 
Matokeo hayo yalikatisha mfululizo wa mechi 11 bila Atletico kupoteza kwenye ligi hiyo wakiwa wameshinda nane na kutoka sare mara tatu.

Diego Simeone
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Hata hivyo, Atletico bado hawajapoteza katika michezo 10 ya nyumbani kwenye La Liga wakiwa wameandikisha sare tatu na ushindi mara saba.
 
"Sidhani walinzi wanapaswa kulaumiwa kwa kupoteza mchezo huo kwa sababu goli hilo lilitokana na set-piece," Meneja wa Atletico Diego Simeone alisema punde baada ya mechi hiyo waliyofungwa na Alaves. 
 
"Lakini ikiwa kunao udhaifu katika ulinzi, au katika kulinda mashambulizi ya set-piece, basi ni dhahiri itabidi tuichunguze vizuri hali hiyo na kurekebisha. Lazima tuendelee kuimarika. Tulikuwa na hatua kadhaa katika mchezo wa leo ambapo tulicheza kwa Subira na nina imani na wachezaji hawa.
 
"Siku zote tunasema kunakuwepo nyakati mbaya katika msimu na huenda hii ni mojawapo. Tuna kikosi kizuri, cha uwiano, na tutatathmini kitu gani kinakwenda mrama na kujaribu kutafuta suluhisho.”

Yannick Carrasco
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Wakati huo huo, Barcelona walidhihirisha wanawazidi nguvu zaidi Levante walipowafunga 3-0 nyumbani katika mechi yao ya karibuni kwenye La Liga, mnamo Septemba 26.
 
Ushindi huo uliwapeleka Barcelona kufikisha idadi ya mechi saba bila kupoteza katika ligi hiyo wakiwa wameandikisha sare tat una kushinda mara nne.
 
Barcelona pia hawajapoteza katika mechi za karibuni walizocheza ugenini- wametoa sare tatu na kushinda mara tatu.
 
Mara ya mwisho Atletico na Barcelona kukutana ilikuwa tarehe 8 Mei 2021.

Atletico walifanikiwa kuwabana Barcelona sare ya 0-0 mechi iliyochezwa katika uwanja wa  Nou Camp. 

Takwimu ( Mara tano walizokutana karibuni)

Mechi - 5
Atletico - 2
Barcelona - 1
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 09/29/2021