KATIBU wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema Serikali itachukuwa hatua kwa wale wanatengeneza jezi feki wa klabu na timu za Taifa.
Amesema jambo la jezi feki linasikitisha na hawataishia kuzungumza bali watafanya kwa vitendo kwa wafanya biashara wote ambao wanatengeza jezi feki .
Aliyazungumza hayo katika uzinduzi wa jezi za
timu za Taifa na alisema wanashiriki na TFF, klabu zote pamoja na wazabuni wa jezi kuwashuhurikia watu hao wanaohujumu uchumi kwa kuuza jezi ya Taifa.
“Natoa rai kwa wale wote wanaofanya huo mchezo, wengine ni Jamaa zangu natangaza sitawasaidia wakifanya mchezo wa kuuza jezi feki na tutashuhurika nao. Niwaambie tu mfanyabiashara anayetaka kuuza jezi anatakiwa kufuata sheria,” alisema Msigwa.
Aliwapongeza TFF kuondoa soka mchezo wa kihuni na kuwa kazi inayoheshimiwa na wadhamini kuweka fedha katika mpira kusaidia kuendeleza soka la Tanzania.
“Katika kuhakikisha Mpira wa Tanzania unazidi kuwa bora , Serikali inashurikiana bega kwa bega na Shirikisho kuhakikisha kila timu ya Taifa inakuwa na mdhamini wake.
Niwaombe wafanya biashara kujitokeza kudhamini timu zetu za Taifa zote ikiwemo vijana na wanawake, nilitarajia leo kuona kila timu imepata mdhamini wake, ila sio mbaya kwa sababu tunampango kukutana na TFF kwa ajili ya mchakato huo,” alisema Msigwa.
Rais wa Shirikisho Wallace Karia alisema anaeapongeza Sandalans kwenda kwa muda kupatikana na jezi kabla ya timu zetu hazijaanza mchakato wa mashindano.
Alisema hizi jezi zimebuniwa kwa ubunifu mkubwa na zimeendana na tamaduni ya Taifa yetu ikiwemo rangi ya Blue ikibeba madini na maji.
“Kama tukiamini sehemu zingine basi tuwekea nguvu zetu kwenye Taifa, timu zingine baadae ila Taifa ndio kwanza. Tutacheza Novemba dhidi ya Morocco hivyo jambo hilo kwetu ni kubwa watanzania wanatakiwa kujaza uwanja wakiwa na jezi mpya.
Ninaimani tutawafunga Morocco hapa nyumbani tukitoka Niger, hivyo mechi hiyo watanzania wanatakiwa kujitokeza uwanjani wakiwa na jezi zao, pia jezi hizo tutatumia kwa timu zetu zote za vijana na wanawake,” alisema Karia.
Mkurugenzi wa Sandalans Fashion Wear Limited, Yusuf Omary alisema jezi zitakiwa aina tatu, nyumbani, ugenini na ya akiba, ambazo watanzania wanaweza kuvaa “Kwa sasa watanzania wanatakiwa kununua jezi za timu za Taifa, tuachana na mahaba yetu ya klabu sasa hivi tunatakuwa kupenda cha kwetu.
Naomba nitoe raia kama watanzania wanataka kufanya biashara basi wanatakiwa kuja mezani ili kufuta taratibu na kupata kipata ambacho kinasaidia kuongeza uchumi wa Taifa letu,” alisema Yusuf.
Aliongeza kuwa kupigia mpira unatangazia sehemu kubwa hivyo wanapongeza viongozi wote wa michezo ikiwemo Shirikisho na Wizara inayosimamia michezo kusimamia vizuri sekta hii kwa kufanya michezo kuwa juu.
“Tunatarajia hivi karibuni kufungua duka maalum ambalo litauza jezi na vifaa vya timu zote za timu zetu zote za Taifa, lakini pia zitakuwepo katika maduka ya klabu zote hapa nchini ikiwemo Simba, Yanga na Azam FC,” alisema Mkurugenzi huyo.
Naye Mkurugenzi wa kudhibiti bidhaa bandia, Hadija Ngasongwa alisema wanakuja na kampeni ya pamgusa kuziondoa jezi zote bandia hapa nchini.
Alisema kuna sheria kali kwa mtu anayefanya biashara bandia kwa kulipa faini ya Million 50 na kifungo lakini pia kuteketeza bidhaa hizo.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.