Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 Shriners Children's Open
PGA Tour
TPC at Summerlin
Las Vegas, Nevada, USA
12-15 October 2023
Shindano la gofu la The
Shriners Children's Open 2023 linatarajiwa kung’oa nanga TPC, Summerlin huko Las Vegas, Nevada, Marekani kati ya tarehe 12 na 15 Oktoba.
Kuhusu shindano hilo
Shindano hili liliasisiwa mwaka 1983, miaka 40 iliyopita na lilikuwa shindano la nne katika msururu wa Tour msimu 2019/20 na ufanyika kila mwaka mwezi Oktoba huko Las Vegas.
Shindano hili huandaliwa TPC Summerlin, magharibi mwa kati kati ya Las Vegas ambapo ni futi 2,700 juu ya usawa wa bahari.
Mwaka 2007 ilitangazwa kuwa mipango na maandalizi ya shindano hili itakuwa chini ya hospitali za watoto za Shriners.
Washiriki
Shindano la mwaka huu litajumuisha wachezaji 132 akiwemo bingwa mtetezi Tom Kim ambaye aliibuka na ushindi wa shindano la mwaka jana, Si Woo Kim mshindi wa shindano la 2021, Emiliano Grillo, Ludvig Aberg na Tom Hoge.
Lexi Thompson ambaye ni nyota wa LGPA Tour atakuwa miongoni mwa washiriki vile vile.
Tuzo
Shindano la mwaka huu 2023 la The Shriners Children's Open litakuwa na zawadi ya dola milioni 8.4 huku mshindi akiondoka na kiasi cha dola milioni 1.51.
Mshindi atapata alama 500 za kombe la FedEx na kombe lililoundwa kutumia kioo.
Nukuu
"Shindano la The Shriners Children's Open limekuwa sehemu ya wenyeji wa Las Vegas kwa miaka 40,” alisema mkurugenzi mtendaji wa shindano hilo Patrick Lindsey.
"Ni furaha kubwa kwetu kusherehekea mafanikio haya pamoja na mashabiki wetu na kuwaletea matukio mapya ikiwemo CLUB360.
"Tunatazamia wiki nyingine ya kufana ya gofu mwezi huu wa Oktoba.”
Washindi watano wa mwisho wa Shriners Children's Open
2018 - Bryson DeChambeau (Marekani)
2019 - Kevin Na (Marekani)
2020 - Martin Laird (Scotland)
2021 - Im Sung-jae (Korea Kusini)
2022 - Tom Kim (Korea Kusini)
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.