BAADA ya kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya
Afrika Football League (AFL) kikosi cha Simba kesho watakuwa na kibarua kigumu cha kutafuta pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC.
Simba wanakuwa wenyeji uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakiwakaribisha Ihefu FC ambao hivi karibuni wamemtambulisha kocha mpya kutoka nchini Uganda, Mosses Basena aliyewahi kuwa kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi na timu ya Taifa ya Uganda.
Katika mchezo huo Simba inaingia kusaka alama tatu ili kuendeleza walipoishia kwa kushinda michezo mitano huku Kocha wa Roberto Oliveira
(Robertinho) akizihitaju alama tatu ili kuhitaji kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Kuelekea mchezo huo Robertinho alisema baada ya kutoka nchini Mirsi katika mchezo wa marudiano na Al Ahly na kuondolewa kwenye mashindano wakapata nafasi ya kufanyia kazi changamoto na sasa kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Ihefu FC.
Alisema siku chache zilizopita wasaidizi wake walifanikiwa kuwafatilia Ihefu FC ilipocheza na Coastal Union na kuona wanavyocheza, ubora na madhaifu yao.
“Kila mechi tunahitaji kuwaheshimu wapinzani wetu bila kujali tunacheza na timu inashika nafasi ya ngapi, malengo yetu ni kucheza vizuri na kupata alama tatu ambazo zitaturejesha kwenye nafasi yetu ya kileleni na mwisho wa msimu kutwaa mataji ya ubingwa,” alisema Robertinho.
Alisisitiza kuwa anaweza kufanya mabadiliko kidogo kwa kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajaonekana mara nyingi kwenye mechi ambapo watakuwa wawili au watatu wanaweza kuanza au kuingia kipindi cha pili.
Kuhusu kutompa nafasi Mosses Phiri , Robertinho alisema ni mchezaji mzuri na kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza kulingana na misingi ya program za michezo wanayokwenda kucheza ikiwemo ligi kuu au michuano ya kimataifa.
"Napanga kikosi kulingana na timu ambazo tunaenda kukutana nazo na jinsi ya misingi ya wachezaji niliokuwa nao, hivi leo nikimuweka benchi Baleke
(Jean) wataniuliza kwanini nampa nafasi Phiri na kumuweka benchi?"
alisema Robertinho.
Naye Mwakilishi wa wachezaji wa Simba, Shaban Chilunda alisema ni muhumi kwa sababu wapinzani wao wako vizuri na hakun timu dhaifu kwenye ligi.
Alisema wamefanya maandalizi mazuri, kila mchezaji wanaenda kupambana kuhakikisha wanavuna alama tatu ili kuwapa furaha mashabiki wao ambao wanahitaji soka safi na matokeo jambo tunaenda kulifanya.
“Ihefu FC ni timu nzuri lakini sisi Simba tuko vizuri zaidi, tunaingia kwa heshima lakini lengo letu kubwa ni kuvuna alama tatu muhimu katika mchezo wetu huo,” alisema Chilunda.
Naye Kocha Mkuu wa Simba, Mosses Basena alisema wamejiandaa vizuri kuikabili na Simba, wanatambua wanakutana na timu nzuri na imetoka kwenye mashindano ya AFL.
Alisema anatarajia utakuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwa sababu anafahamu ubora wa timu hiyo ikiwemo safu ya ushambuliaji na ulinzi pia na anaimani ya kuonyesha mpira mzuri.
“Kwa wiki mbili tangu nimekabodhiwa kukinoa kikosi cha Ihefu FC kuna jambo nimeweza kulifanya ninaimani tutaonyesha upinzani mkubwa mbele ya Simba,” alisema Basena.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.