Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo
KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewabadilishia programu wachezaji wake kulingana na ubora wa Azam FC ambao watakutana nao katika
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, mwaka huu, Yanga watakuwa wenyeji wakiwakaribisha Azam FC , uwanja wa Azam,Chamazi Dar-es-Salaam.
Kocha Gamondi alisema licha ya kutokamilika kwa wachezaji wote ameanza mazoezi ya nguvu na nyota waliopo wanakuwa imara kila upande.
Alisema anatambua ubora wa Azam FC lakini hawatokubali kupoteza mchezo huo ambao utakuwa wa ushindani mkubwa kwa sababi ya kila mmoja anahitaji alama muhimu.
“Kila mchezaji anatambua wajibu wake, tupo vizuri kila nafasi na tunaendelea kuwa imara katika sehemu chache ikiwemo ulinzi na ushambuliaji ambazo zilikuwa na kasoro.
"Kikubwa tunataka ushindi wa mbao mengi mbele ya Azam FC, naamini hata wapinzani wanafanya maandalizi, kwetu tunahitaji kuingia kwa mbinu tofauti na michezo iliyopita kwa sababu tunahitaji kutetea taji,”
alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa hawatoruhusu kupoteza mchezo wa pili kwenye ligi ikiwa mbichi ndio wakati wa kutafuta matokeo mazuri katika kila mechi zilizopo mbele yao bila ya kujali wanacheza ugenini au nyumbani.
Gamondi alisema kila mechi inekuwa na maandalizi yake na kuelekea mchezo huo wanajiandaa kulingana na ubora wa Azam FC ambao wamekuwa nao kwa sasa.
KIGOGO YANGA AWAPIGA MKWARA WAARABU.
MAKAMU wa Rais Yanga, Arafat Haji ametamba wana kikosi kizuri ambacho kinaweza kushindana na timu kubwa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Arafat alisema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha Egyptian Tv kwamba katika mchezo dhidi ya Al Ahly wapo tayari kupambana nao na kuhakikisha wanapata matokeo nyumbani na ugenini lakini watafanya hivyo kwenye michezo mingine ya kundi D.
Arafat alisema wamekuwa wakicheza kwa kujiamini na wanajua wanakutana na timu kubwa kama Al Ahly ambao wanatetea ubingwa, lakini wanaamini kuwa nao wana kikosi kizuri.
“Al Ahly ni timu nzuri na itakuwa inatetea ubingwa. Sisi tunatakiwa kuonyesha kwamba tunastahili kushindana nao na kushinda mechi ya nyumbani na ugenini,” alisema Arafat.
Alisema kama uongozi siku zote wameendelea kulipa benchi la ufundi kila hitaji na wapo tayari kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa.
“Timu yetu ipo tayari kwa Ligi ya Mabingwa. Tuna wachezaji katika timu ya Taifa Tanzania na wapo wachezaji wengine wenye uzoefu wa kutosh.
Tunaamini tunaweza kufanya vizuri kwenye michezo yetu ya kundi,”
alisema.
Yanga katika kundi la Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza kutupa karata yake ya kwanza Novemba 24 dhidi CR Belouizdad ikiwa ugenini nchini Algeria kisha itatupa karata hapa nchini Desemba Mosi kwa kuikaribisha Al Ahly.
Katika kundi Yanga ipo na timu za CR Belouizdad, Medeama na Al Ahly.
Shinda Smartphone Mpyaa
Jisajili, Beti na Ushinde HUAWEI NOVA 9 MPYAA! Kila wiki, tunatoa Mshindi wa Simu kwa wiki 5 mfululizo kuanzia Oktoba 5.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.