Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 9
Chelsea v Arsenal
Stamford Bridge
London, England
Saturday, 21 October 2023
Arsenal itapambana na Chelsea katika
mechi ya ligi ugani Stamford Bridge Jumamosi Oktoba 21. Mechi hii itakuwa yao ya nne dhidi ya timu zilizopo mjini London zinazoshiriki ligi kuu.
The Gunners waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace ugani Selhurst Park katika mkondo wa pili wa ligi msimu huu kabla ya kutoa sare ya 2-2 dhidi ya Fulham na Tottenham mtawalia.
Arsenal chini ya Mikel Arteta walipata ushindi wa pili ndani ya miezi mitatu dhidi ya Manchester City walipoibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani huku ushindi wa kwanza wakiupata katika mechi ya Ngao ya Jamii maarufu kama Community Shield.
The Gunners hawajapoteza mechi hata moja ya ligi msimu huu na sasa wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Spurs kwa ubora wa magoli baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Luton ugani Kenilworth Road.
Alamy hisa picha
Baada ya wakati mgumu, the Blues wanaonekana kuimarika chini ya mkufunzi Mauricio Pochettino baada ya kuandikisha ushindi wa mechi mbili mfululizo; 2-0 dhidi ya the Cottagers na 4-1 dhidi ya Burnley kwa mara ya kwanza tangu raia huyo wa Argentina kutwaa mikoba ya kufundisha timu hiyo.
Kwa sasa Chelsea wanashikilia nafasi ya 11, alama moja nyuma ya Manchester United (10) na alama sita chini ya nafasi za kushiriki kombe la UEFA Champions League.
Wilson Odobert aliwapa bao la uongozi Burnely ugani Turf Moor dhidi ya Chelsea dakika ya 15. Raheem Sterling alionyesha mchezo wa kufurahisha katika mechi hiyo na kuchangia kupatikana kwa magoli yote manne ya Chelsea huku yeye akifunga goli moja dakika ya 65.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Eddie Nketiah alicheza mchezo mzuri dhidi ya Citizens na kutatiza safu yao ya ulinzi japokuwa hakufanikiwa kufunga bao lolote. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliondolewa uwanjani dakika ya 75 na sasa ni mechi tano bila goli kwa mshambuliaji huyo.
Pochettino anaamini kuwa mshikamano anaokuza katika kikosi hicho utazaa mafanikio hizi karibuni huku akikiri kuwa majeraha kwa wachezaji muhimu yameathiri mafanikio.
"Lengo ni kutengeneza kikosi kizuri na kuleta uhiano. Ni wachezaji wachanga wanaohitaji muda wa kuelewana uwanjani,” aliambia Chelsea TV. "Hili litafanikiwa kupitia mazoezi na kukipa kikosi muda. Hakuna shaka kuwa baada ya muda hali itakuwa ya kuridhisha.
"Umakini unahitajika tunapo hukumu timu na wachezaji. Tunazidi kukua na kuimarika na mafanikio yanakuja japokuwa tunakumbwa na changamoto wakati mwingine. Kwa pamoja tutafanikiwa mwisho wa safari.
"Tunawakosa wachezaji muhimu wanaoweza kutusaidia kuimarika kwa muda mfupi. Majeruhi wakipona tutakuwa tayari kupigania mataji makubwa.”
Arteta alifurahi kupata ushindi dhidi ya City hatimaye baada ya mechi sita katika ligi bila mafanikio na anaamini kuwa ni ishara tosha kuhusu udhabiti wao.
"Ni ujumbe tosha kwa kikosi hiki kuzidi kujituma hata zaidi,” alisema raia huyo wa Uhispania. “City ina kikosi imara kinachoelewana vizuri uwanjani. Sio rahisi kushindana nao. Unahitaji jitihada za ziada.
"Nina furaha sana leo, nilikuwa na furaha Jumatano tulipopoteza mchezo wetu na vile vile najivunia kuwa sehemu ya kikosi hiko leo kwa kuwa sisi ni timu.”
Takwimu baina ya timu hizi mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Chelsea - 1
Arsenal - 4
Sare - 0
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 9:
Jumamosi, Oktoba 21
2:30pm: Liverpool v Everton
5:00pm: Bournemouth v Wolverhampton Wanderers
5:00pm: Brentford v Burnley
5:00pm: Manchester City v Brighton & Hove Albion
5:00pm: Newcastle United v Crystal Palace
5:00pm: Nottingham Forest v Luton Town
7:30pm: Chelsea v Arsenal
10:00pm: Sheffield United v Manchester United
Jumapili, Oktoba 22
6:30pm: Aston Villa v West Ham United
Jumatatu, Oktoba 23
10:00pm: Tottenham Hotspur v Fulham
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.