EPL - Arsenal v Manchester City


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 English Premier League
Matchday 8

Arsenal v Manchester City

Emirates Stadium
London, England
Sunday, 8 October 2023
Kick-off is at 17h30 CAT
 
Manchester City watakabiliana na Arsenal katika mechi ya ligi ugani Emirates mnamo Jumapili Oktoba 8.
 
The Citizens walimiliki mpira kwa kipindi kirefu ugani Molineux dhidi ya Wolves bila mashambulizi yoyote makubwa kwenye lango la wapinzani Septemba 30 ambapo wenyeji waliibuka na ushindi wa 2-1.
 
City chini ya Pep Guardiola wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la ligi, alama moja juu ya Tottenham na the Gunners wanaoshikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia wakitofautiana kwa ubora wa magoli.

Martin OdegaardHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Arsenal na Tottenham wapo juu ya Liverpool kwa alama moja katika nafasi ya 4 huku Aston Villa wakiingia tano bora baada ya kuibuka na ushindi wa 6-1 dhidi ya Brighton Villa Park.
 
Arsenal ambao ni mabingwa wa kombe la Community Shield 2023 walipata ushindi wa 4-0 dhidi ya the Cherries ugani Vitality Stadium, ambapo Kai Havertz alipata bao lake la kwanza akiwa na timu ya Arsenal.
 
Martin Odegaard amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu wa 2023-24 wa ligi na alihusika kwa njia moja au nyingine katika kupatikana magoli yote manne. Alifunga penalti dakika ya 44 na kusaidia goli la Ben White katika dakika za nyongeza. Awali kwenye mechi hiyo, raia huyo wa Norway alisaidia goli la Gabriel Jesus kabla ya kuangushwa katika kisanduku na kusababisha penalti iliyofungwa na Havertz.
 
Julian Alvarez
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Julian Alvarez aliifungia City goli la kusawazisha katika dakika ya 58 baada ya mchezaji wao kuchezewa vibaya. Licha ya kumiliki mpira kwa kipindi kirefu kwenye mchezo huo, City hawakushambulia kama walivyozoeleka. Bao la Alvarez lilikuwa lake la kwanza katika michezo mitatu, na amefikisha idadi ya magoli 3 msimu huu baada ya michezo saba.
 
Arteta anaamini kuwa goli la Havertz litachochea uchu zaidi baada ya wengi kumtupia lawama raia huyo wa Ujerumani kwa uchezaji wake katika mechi zake sita za kwanza.
 
"Goli hilo litabadilisha mambo mengi. Hakuna mjadala katika swala la hisia na mapenzi yetu kwake. Tunadhamini sana mchango wake kwetu.” Alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Mwanariadha maarufu Usain Bolt aliwai kusema, ‘nafanya mazoezi kwa kipindi cha miaka minne ili kukimbia sekunde tisa’, muda mwingine unajituma sana ila inawezekana usione hilo. Baada ya goli hili, wakati mgumu aliopitia wiki chache zilizopita atafarijika.”
 
Huku akitumikia marufuku, Guardiola hakuruhisiwa kwenye eneo la ufundi na alifuatilia mechi hiyo kutoka jukwaa la mashabiki. Kocha huyo alikiri kuwa Wolves walikuwa bora kuliko timu yake walipokuwa wanashambulia hasa pembezoni mwa uwanja.
 
"Hatukuwa na mtiririko katika mashambulizi yetu na ndiyo sababu ya kutopata mafanikio,” alisema Guardiola. “Neto alituzidi maarifa.
 
"Walitudhibiti sio kwa sababu tulikosa mwelekeo ila kwa sababu walikuwa bora nyakati tulizotakiwa kuzuia. Tulifahamu utakuwa mchezo mgumu na walionyesha mchezo mzuri sana. Pongezi kwa Wolves.”
 
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Arsenal - 0
Man City - 5
Sare - 0
 
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 8.
 
Majira ya Afrika ya Kati
 
Jumamosi, Oktoba 7
 
1:30pm: Luton Town v Tottenham Hotspur
 
4:00pm: Burnley v Chelsea
 
4:00pm: Everton v Bournemouth
 
4:00pm: Fulham v Sheffield United
 
4:00pm: Manchester United v Brentford
 
6:30pm: Crystal Palace v Nottingham Forest
 
Jumapili, Oktoba 8
 
3:00pm: Brighton & Hove Albion v Liverpool
 
3:00pm: West Ham United v Newcastle United
 
3:00pm: Wolverhampton Wanderers v Aston Villa
 
5:30pm: Arsenal v Manchester City
 

Shinda Smartphone Mpyaa

Jisajili, Beti na Ushinde HUAWEI NOVA 9 MPYAA! Kila wiki, tunatoa Mshindi wa Simu kwa wiki 5 mfululizo kuanzia Oktoba 5.


 
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 10/06/2023