Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIA Formula One World Championship
2022 Mexican Grand Prix
Autodromo Hermanos Rodriguez
Mexico City, Mexico
Sunday, 30 October 2022
Max Verstappen wa Red Bull Racing anatarajia kupata ushindi wake wa 14 wa msimu ambao utakuwa ni rekodi Oktoba 30 Jumapili kwenye mbio za
Mexican Grand Prix.
Ushindi wa mbio za United States Grand Prix wa raia huyo wa Uholanzi ulipelekea kushika rekodi iliyokuwa imeshikiliwa na Michael Schumacher na Sebastian Vettel waliopata mafanikio hayo mwaka 2004 na 2013 mtawalia.
Verstappen aliingia kwenye vitabu vya historia alipotetea taji lake la dunia kwa mafanikio aliposhinda mbio za Japanese Grand Prix, huku mafanikio hayo ya kutetea ubingwa kwa mafanikio yakiafikiwa na madereva 12 tu.
Red Bull Racing walipata ubingwa wa dunia wa waundaji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013 kwenye mkondo wa the Americas ambao ulikuwa ni ushindi wao wa tano kwa ujumla. Ushindi huo ulivunja msururu wa ushindi wa timu ya Mercedes.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kiongozi wa timu, Christian Horner alisema ushindi huo ni kwa ajili ya mwanzilishi wa RedBull Dietrich Mateschitz ambaye aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa 78.
"Imekuwa wikendi iliyojawa na hisia. Ulikuwa ni wakati mwafaka kwetu kushinda mbio hizi. Nahisi Dietrich atakuwa mwenye furaha kwa ushindi huu,” Horner aliambia kituo cha Sky Sports.
"Max alihitaji kupambana zaidi baada ya kuwa na shida ya gurudumu la mbele.
"Alijituma sana. Nilifahamu matokeo yatakuwa kama yalivyokuwa katika mbio hizi. Kushinda taji la dunia la waundaji baada ya miaka nane ni mafanikio makubwa.
"Ina maana kubwa kwetu. Imekuwa safari ndefu kufika hapa. Dietrich alikuwa msiri sana ila alifurahia maisha, michezo na hasa mbio za Formula 1. Alikuwa na ndoto ya kumiliki timu ya Formula 1.
"Alifanikiwa kufanya hivyo. Alimiliki timu mbili na alitupa nafasi sisi sote. Aliamini katika uwezo wetu na kutuunga mkono na ushindi huu ni kwa ajili yake. Tunamshukuru sana kwa yote aliyotufanyia; binafsi na timu. Usiku wa leo tunamuenzi.”
Alipoulizwa kilichokuwa kikiendelea akilini mwake alipopata hitilafu Austin, Verstappen alisema, “maneno mengi ya lugha isiyofaa. Nilikuwa nimekasirika sana lakini mara baada ya kubonyeza kidude cha kudhibiti kasi, sharti ufanye juhudi zaidi kwa lengo la ushindi.
"Haikuwa rahisi. Bahati nzuri mkondo huu ni mzuri kwa mbio tofauti na baadhi ya mikondo mingine ambapo ingekuwa sawa na mbio kukamilika. Huu ni mkondo mzuri sana.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa sasa, madereva wengine wanapigania nafasi ya pili ya ubingwa wa dunia kwa madereva huku dereva wa Ferrari Charles Leclerc 267 akiwa alama mbili mbele ya Sergio Perez wa Red Bull Racing mwenye alama 265, baada ya kumshinda raia huyo wa Mexico kwenye mbio za United States Grand Prix.
Leclerc amemaliza katika nafasi ya jukwaani mara tano mfululizo msimu huu katika mbio zake tano za mwisho huku akipata ushindi wa mbio tatu.
Matokeo ya mbio za United States Grand Prix 2022
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Charles Leclerc - Ferrari
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.