Verona kuwaalika mabingwa Milan


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A 

Matchday 10

Hellas Verona v AC Milan 

Stadio Marc'Antonio Bentegodi 
Verona, Italy
Sunday, 16 October 2022
Kick-off is at 21h45  
 
Hellas Verona watakabiliana na mabingwa wa ligi ya Italia AC Milan kwenye mechi ya ligi ugani Stadio Marc'Antonio Bentegodi Oktoba 16.
 
The Yellow and Blues, ambao ni Hellas Verona walishindwa kwenye 2-1 kwenye mechi iliyoipta ya ligi wakiwa ugenini dhidi US Salernitana Oktoba 9.
 
Kwa sasa, Verona hawajapata ushindi wowote kwenye mechi nne za ligi zilizopita huku wakipoteza mechi zote nne mfululizo.

Ante Rebic
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
The Yellow and Blues walikuwa wamepoteza mechi mbili za ligi kati ya mechi tatu walizocheza, huku wakipata ushindi kwenye mechi dhidi ya UC Sampdoria kabla ya kukutana na Salernitana.
 
Kwa upande mwingine, Milan walipata ushindi wa 2-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Juventus FC kwenye mechi ya mwisho ya ligi Oktoba 8.
 
Rossoneri hawajashindwa kwenye mechi mbili zilizopita za ligi baada ya kuandikisha ushindi kwenye mechi mbili mfululizo.
 
Vile vile, Milan hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi 16 wakiwa ugenini huku wakiandikisha ushindi mara 11 na kupata sare tano.
 
“Tulionyesha ushirikiano mkubwa kwenye mechi ya leo. Hatukufanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Chelsea mjini London na tulifanya maamuzi duni dhidi ya mpinzani bora,” alisema meneja wa Milan Stefano Pioli.
 
"Tukicheza kwa ushirikiano tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri. Hatukupata matokeo tuliyotaka London kwa kuwa hatukucheza kwa kasi na tulifanya makosa mengi binafsi yaliyowezesha Chelsea kutuadhibu.
 
“Huu ulikuwa mchezo muhimu wa ligi hasa kwa sababu ni Milan dhidi ya Juventus. Tulipambana vizuri tangu mwanzo wa mechi.”
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Verona na Milan ilikuwa mwezi Mei 8 2022.
 
Milan walipata ushindi wa 3-1 dhidi Verona kwenye mechi ya kusisimua iliyochezewa ugani  Stadio Marc'Antonio Bentegodi.
 

Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi 5 za ligi zilizopita.

Mechi - 5
Verona - 0
Milan - 3
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 10.

 
Oktoba 15 Jumamosi.
 
4:00pm - AC Monza v Empoli FC 
 
7:00pm - Torino FC v Juventus FC
 
9:45pm - Atalanta BC v US Sassuolo 
 
Oktoba 16 Jumapili
 
13h30 - Inter Milan v US Salernitana 
 
4:00pm - SS Lazio v Udinese Calcio 
 
4:00pm - Spezia Calcio v US Cremonese 
 
7:00pm - SSC Napoli v Bologna FC 
 
9:45pm - Hellas Verona v AC Milan 
 
Oktoba 17 Jumatatu
 
7:30pm - UC Sampdoria v AS Roma 
 
9:45pm - US Lecce v ACF Fiorentina 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.


Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 10/14/2022