Roma na Napoli kukutana kwenye dabi del Sole


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 11

AS Roma v SSC Napoli

Stadio Olimpico 
Rome, Italy 
Sunday, 23 October 2022 
Kick-off is at 21h45 
 
AS Roma itakuwa mwenyeji wa SSC Napoli katika mechi ya ligi kuu Italia mnamo Oktoba 23 ugani Stadio Olimpico.
 
Wakiwa nyumbani, Roma walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya US Lecce katika mechi ya ligi iliyopita Oktoba 9 na watakuwa ugenini dhidi ya UC Sampdoria Oktoba 17.
 
Roma hawajapoteza mchezo wowote wa ligi katika mechi mbili zilizopita huku wakiandikisha ushindi kwenye mechi mbili mfululizo.

Stephan El ShaarawyHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Roma wameshinda mechi mbili kati ya mechi tatu za ligi za mwisho wakiwa nyumbani huku wakipoteza mechi ya tatu dhidi ya Atalanta BC kabla ya kukutana na Lecce.
 
Kwingineko, Napoli walipata ushindi wa 3-2 nyumbani dhidi ya Bologna FC kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi Oktoba 16.
 
Napoli wamecheza mechi 14 za ligi bila kupoteza mechi yoyote huku wakiandikisha sare mbili na kupata ushindi wa mechi kumi na mbili.
 
Vile vile, Napoli hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi saba za mwisho walizocheza ugenini huku wakipata ushindi wa mechi sita na sare moja.

Luciano SpallettiHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
 “Nilifurahi kuona hata baada ya kufanya makosa, wachezaji wangu walikuwa wakitafuta mpira na kumdhibti mpinzani,” alisema meneja wa Napoli Luciano Spalletti baada ya ushindi dhidi ya Bologna.
 
"Ilinifanya kuhisi fahari kuwa kocha wa wachezaji hawa. Kwa mara nyingine, wachezaji wa akiba walioingia uwanjani walisaidia timu kwa maamuzi yao kwenye mchezo.  
 
"Juhudi za kila mchezaji zinahitajika na ni muhimu. Wachezaji wa akiba wana mchango mkubwa.”
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Roma na Napoli ilikuwa mnamo Aprili 18 2022.
 
Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 na ilichezewa ugani Stadio Diego Armando Maradona ambao una uwezo wa kubeba mashabiki 60,240.
 
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Roma - 0
Napoli - 3
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 11. 

 
Oktoba 21 Ijumaa
 
9:45pm - Juventus FC v Empoli FC 
 
Oktoba 22 Jumapili
 
4:00pm - US Salernitana v Spezia Calcio 
 
7:00pm - AC Milan v AC Monza
 
9:45pm - ACF Fiorentina v Inter Milan
 
Oktoba 23 Jumapili
 
13h30 - Udinese Calcio v Torino FC 
 
4:00pm - Bologna FC v US Lecce 
 
7:00pm - Atalanta BC v SS Lazio 
 
9:45pm - AS Roma v SSC Napoli
 
Oktoba 24 Jumatatu
 
9:45pm - US Cremonese v UC Sampdoria 
 
9:45pm - US Sassuolo v Hellas Verona 
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 
 
 

Published: 10/20/2022